Afisa Msimamizi wa Uchaguzi Kituo cha Old Kibra Alikopiga Kura Raila Apoteza fomu 34A

Kituo cha shule ya msingi ya Old Kibra ndicho kituo ambacho Raila Odinga alipiga kura yake Jumanne.

Muhtasari

• Afisa Msimamizi katika kituo cha kupigia kura cha mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga amepoteza fomu yake ya awali ya 34A.

Picha: ENOS TECHE
Picha: ENOS TECHE

Afisa Msimamizi katika kituo cha kupigia kura cha mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga amepoteza fomu yake ya awali ya 34A.

 

Katika video iliyoonekana kusambazwa mitandaoni, Afisa huyo msimamizi ambaye alikuwa akiwaeleza mawakala katika kituo cha kujumlisha kura eneo bunge la Kibera huko Upper hill alisema alipoteza fomu hizo alipokuwa akihamisha karatasi zake za kupigia kura ili ziidhinishwe katika kituo cha kujumlisha kura.

David Diang'a, ambaye alikuwa Mkuu wa Ofisi ya Mkondo 8 katika kituo cha kupigia kura cha Old Kibera, alisema kuwa alikuwa na hati hizo ambazo zilikuwa kwenye bahasha.

"Nilikuwa nazo kwenye bahasha na nilikuwa na begi na nikiwa nasimamia kura zangu lakini nikiwa nazisukuma humu ndani ili nipate kibali, lakini nilipofika hapa kwa bahati mbaya sikuwa na fomu," anasikika akijieleza.

Hata hivyo Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo alisema atategemea takwimu walizozipata na kuongeza kuwa sheria inaruhusu kufunguliwa tena kwa kura hizo, lakini mbele ya mawakala waliopo.

Aliongeza kuwa PO itapatikana kujibu maswali yoyote ambayo yanaweza kuhitaji ufafanuzi.

Shule ya msingi ya Old Kibra ndicho kituo ambacho Jumanne kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga alipiga kura yake baada ya kupokelewa kishujaa na mamia ya wafuasi wake waliojitoma pale kwa mamia kushuhudia  kiongozi huyo akitekeleza wajibu wake wa kidemokrasia kuwachagua viongozi kama Mkenya yeyote yule.