Mohammed Ali ahifadhi kiti cha Mbunge wa Nyali

Matokeo hayo yalitangazwa na afisa mrejeshaji kura katika eneo bunge la Nyali John ole Taiswa

Muhtasari
  • Ali alipata kura 32,988 dhidi ya mpinzani wake mkuu Said Abdalla almaarufu Saido wa ODM aliyepata 18,642
Mohammed Ali
Mohammed Ali
Image: image:Hisani

Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amehifadhi kiti chake katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi punde.

Ali alipata kura 32,988 dhidi ya mpinzani wake mkuu Said Abdalla almaarufu Saido wa ODM aliyepata 18,642.

Matokeo hayo yalitangazwa na afisa mrejeshaji kura katika eneo bunge la Nyali John ole Taiswa katika kituo cha kujumlisha kura za eneo bunge hilo, Mamlaka ya Kitaifa ya Mafunzo ya Viwanda (Nita) Mombasa.

Wapinzani wanne walikuwa wanawania kiti hicho cha mbunge wa nyali katika uchaguzi mkuu..

Moha aliwashukuru wafuasi wake katika hotuba yake ya kukubalika akiwaahidi kuwa atafanya kile alichoahidi wakati wa kampeni.

“Nataka kuwashukuru kwa kunichagua, wale tulikua tunashindana nao sasa ni wakati wa kuchapa kazi pamoja,” alisema.