logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sina shida kupoteza kiti cha Mbunge wa Kieni mradi Raila ashinde!- Kanini Kega

Kega alipoteza kiti cha ubunge wa Kieni kwa Antony Njoroge Wainaina wa UDA.

image
na SAMUEL MAINA

Uchaguzi11 August 2022 - 18:31

Muhtasari


  • •Kanini tayari amekubali kushindwa na kutangaza kuwa atakuwa anaangazia mambo mengine baada ya kutimuliwa.
  • •Ameweka wazi kuwa hana shida kupoteza kiti cha ubunge wa Kieni mradi tu mgombea urais wa Azimio-One Kenya apate ushindi.
Mbunge wa Kieni anayeondoka Kanini Kega

Mbunge wa Kieni anayeondoka Kanini Kena amebainisha kuwa tayari amekubali hatima yake baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Agosti 9.

Matokeo ya ubunge wa kieni yaliyotangazwa Jumatano yaliashiria kuwa Mkurugenzi huyo wa  uchaguzi wa Jubilee amepoteza kiti kwa Antony Njoroge Wainaina ambaye alikuwa anawania kwa tiketi ya UDA.

Kufuatia hayo Kanini tayari amekubali kushindwa na kutangaza kuwa atakuwa anaangazia mambo mengine baada ya kutimuliwa.

"Nafungua ukurasa mpya, mlango mmoja ukifungwa mwingine hufunguliwa. Naelekea Bomas," Kanini alisema kupitia Facebook siku ya Jumatano.

Baadae siku hiyo alielekea katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura huko Bomas of Kenya ili kufuatilia hesabu za kura ya urais.

Kanini sasa ameweka wazi kuwa hana shida kupoteza kiti cha ubunge wa Kieni mradi tu mgombea urais wa Azimio-One Kenya apate ushindi.

"Jinsi nilivyopeza maisha haya nyororo. Sina shida na kupoteza kiti cha ubunge wa Kieni lakini Baba the 5th ashinde!" Kega alisema.

Mbunge huyo kwa mihula ya pili alieleza imani yake kuwa muungano wa Azimio utatwaa uongozi wa taifa kufuatia uchaguzi wa Jumanne.

"William Ruto na Rigathi Gachagua mlidanganya watu wetu na sasa watakuwa upinzani kwa miaka 5 ijayo! Tutarudia tena!" Alisema.

Kega na miongoni mwa wandani wa rais Uhuru Kenyatta ambao walipoteza viti vya katika eneo la Mt Kenya katika uchaguzi wa mapema wiki hii. Wengine ni pamoja na Wambugu Ngunjiri, Amos Kimunya, Jeremiah Kioni na wengineo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved