logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jubilee yalalamika kuhusu wizi wa kura katika maeneo bunge 33 ya Mt Kenya

Kioni alitupilia mbali dhana kwamba kuna wimbi la UDA katika eneo la Mlima Kenya  lililowafagia wapinzani wao.

image
na

Habari11 August 2022 - 21:44

Muhtasari


•Jubilee inadai kuwa kulikuwa na wizi wa kura za kupendelea mpinzani wao UDA katika maeneo bunge ya Mlima Kenya.

•Kioni alisema maajenti wao walisema kulikuwa na rushwa, vitisho na maonyesho ya vifaa vya kampeni za UDA

Chama cha Jubilee sasa kinadai kuwa kulikuwa na wizi wa kura za kupendelea mpinzani wao UDA katika maeneo bunge ya Mlima Kenya.

Haya ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa chama hicho Jeremiah Kioni siku ya Alhamisi.

Kioni alitupilia mbali dhana kwamba kuna wimbi la UDA katika eneo la Mlima Kenya ambalo liliwafagia wapinzani wao.

"Kwa rekodi, wacha sote na wengine tujue kuwa hakukuwa na "Mawimbi ya Manjano" katika eneo la Mlima Kenya ikiwa ni pamoja na mikoa mingine kama Bungoma, Taita Taveta na Kisii. Madai haya yako mbali na ukweli," taarifa hiyo ilisema.

"Tumejifunza kuhusu mpango mkubwa wa udanganyifu ambao ulifanyika katika maeneo bunge 33 ya Mlima Kenya kwa kiti cha ubunge."

Kioni alisema maajenti wao katika vituo vya kupigia kura vya maeneo hayo walisema kulikuwa na rushwa, vitisho na maonyesho ya vifaa vya kampeni za UDA ndani ya mipaka ya vituo hivyo.

Pia walisema kulikuwa na ubadhirifu wa maajenti wa Azimio na maafisa wasimamizi.

Hii ilikuwa kwa kuwazuia nje ya vituo vya kupigia kura kwa wakati.

"Maajenti walipata bahasha zisizoweza kuharibiwa zenye mihuri bila kufungwa," Kioni alisema.

"Idadi ya wapiga kura katika KIEMs haikulingana na idadi ya vizuizi vya kura vilivyotumika," aliongeza.

Jubilee inadai zaidi kuwa kulikuwa na ukosefu wa ufafanuzi kuhusu uthibitishaji wa wapigakura ambapo vifaa vya KIEMs vilifeli.

Kioni alisema watatangaza hatua ambayo watachukua kufuatia madai hayo.

Pia aliwafariji wagombea ubunge wa Azimio walioshindwa katika eneo hilo.

Kioni ni miongoni mwa wanasiasa walioshindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Mbunge huyo wa Ndaragwa alikubali kushindwa na George Gachagua wa UDA.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved