IEBC yatoa orodha mpya ya watu watakaoruhusiwa Bomas

Maafisa wa usalama wametumwa katika kituo hicho ili kuimarisha agizo hilo

Muhtasari

•Mabadiliko ambayo yalitangazwa na kamishna Abdi Guliye yatawafanya baadhi ya waliokuwepo ukumbini kuondoka.

Maafisa zaidi wa polisi waliongezwa kwenye jumba hilo baada ya kamishna wa IEBC Abdi Guliye kuamuru watu wasio wa muhimu kutoka katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura, Bomas of Kenya mnamo Agosti.
Maafisa zaidi wa polisi waliongezwa kwenye jumba hilo baada ya kamishna wa IEBC Abdi Guliye kuamuru watu wasio wa muhimu kutoka katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura, Bomas of Kenya mnamo Agosti.
Image: ANDREW KASUKU

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) imefanya mabadiliko kuhusu watu watakaoruhusiwa katika kituo cha kujumuisha kura cha kitaifa katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

Mabadiliko ambayo yalitangazwa na kamishna Abdi Guliye yatawafanya baadhi ya waliokuwepo ukumbini kuondoka.

“Tumefanya mabadiliko ya watakaoruhusiwa katika kituo cha kujumlisha kura cha Bomas, tutaruhusu tu kuwepo kwa mawakala, watu watakaowasaidia, mawakala wakuu, naibu mawakala wakuu, makarani, waangalizi na vyombo vya habari unavyoweza kuandika utakavyo,” alisema. 

"Kuanzia sasa, ikiwa hauko kwenye terrace, tafadhali unaweza kutafuta njia yako ya kutoka."

Maafisa wa ziada wa usalama wametumwa katika kituo hicho ili kuimarisha agizo hilo.