Seneta wa sasa wa Narok, Ledama Olekina amechaguliwa tena kuhudumu kwa muhula mwingine ofisini.
Ledama alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 135,180.
Alikuwa akigombea kwa tiketi ya chama cha Orange Democratic Movement (ODM).
Samuel Tunai ambaye alikuwa mshindani wake wa karibu alishika nafasi ya pili kwa kura 117,869.
Tunai aligombea kwa tiketi ya chama cha UDA.
Seneta huyo aliyeko madarakani alikuwa miongoni mwa wawaniaji waliopewa tikiti ya moja kwa moja na chama cha ODM.
Ledama anaenda kuhudumu kwa mara ya pili kama seneta.