Uchaguzi 2022: Orodha ya magavana waliozoa ushindi

Utangazaji wa matokeo ya viti vya ugavana ulianza Alhamisi, Agosti 11.

Muhtasari

• Kati ya Kaunti 47, ni Kaunti 45 pekee zilizoshiriki uchaguzi kwa viti vyote sita vya kuchaguliwa.

• Kaunti za Mombasa na Kakamega, hata hivyo, hazikushiriki katika uchaguzi wa ugavana.

Image: RADIO JAMBO

Wakenya kote nchini walipiga kura zao kwa viti mbalimbali vya uchaguzi Jumanne, Agosti 9.

Upigaji kura ulimalizika kwa amani na kufikia wakati wa kuchapishwa, matokeo ya Wabunge wa Bunge la Kitaifa na yale ya bunge la kaunti yalikuwa yametangazwa.

Kati ya Kaunti 47, ni Kaunti 45 pekee zilizoshiriki uchaguzi wa viti vyote sita vya kuchaguliwa.

Kaunti za Mombasa na Kakamega, hata hivyo, hazikushiriki uchaguzi wa ugavana.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisitisha zoezi hilo baada ya mkanganyiko wa uchapishaji wa karatasi za kura.

Alisema karatasi za kupigia kura za maeneo hayo zilikuwa na picha na maelezo yasiyo sahihi ya wagombea.

Baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura Jumanne, utangazaji wa matokeo ya viti vya ugavana ulianza Alhamisi, Agosti 11.

Haya hapa ni baadhi ya matokeo yaliyopokelewa na Radio Jambo.

1. Kaunti ya West Pokot

Mgombea wa chama cha UDA Simon Kachapin alishinda baada ya kujizolea kura 86,476. Gavana aliye madarakani John Lonyangapuo aliibuka wa pili kwa kura zaidi ya 84,610.

2. Kaunti ya Trans Nzoia

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, George Natembeya ameshinda ugavana baada ya kupata kura 158,919.

Mshindani wake Chris Wamalwa wa Ford Kenya aliibuka wa pili kwa kura 79,020.

3. Kaunti ya Isiolo

Abdi Hassan Guyo wa chama cha Jubilee ameshinda kiti hicho baada ya kupata kura 28,946.

Alimshinda mpinzani wake mkuu Godana Doyo aliyepata kura 2,551 kama mgombea huru.

4. Kaunti ya Siaya

Seneta anayeondoka James Orengo ameshinda ugavana kwa kura 220,349 akimshinda mshindani wake Nicholas Gumbo aliyeibuka wa pili kwa kura 147,558.

5. Kaunti ya Nandi

Stephen Sang amehifadhi kiti chake baada ya kupata kura 237,045.

Mgombea huyo wa UDA alimshinda mpinzani wake aliyekuwa Gavana Cleophas Lagat ambaye alipata kura 54,375.

6. Kaunti ya Busia

Chama cha ODM kilidumisha kiti hicho kupitia Paul Otuoma aliyepata 164,478. Mgombea wa ANC John Sakwa aliibuka wa pili kwa kura 92,144.

7. Kaunti ya Migori

Ochilo Ayacko wa ODM alishinda kiti hicho kwa kura 175,226. Mpinzani wake wa DAP-K John Pesa alifuata mkia kwa kura 126,171.

8. Kaunti ya Marsabit

Mohamud Ali wa UDM amefanikiwa kuhifadhi kiti chake baada ya kupata kura 38,803 na kumshinda mgombea wake wa karibu wa KANU na mbunge wa zamani wa North-Horr Francis Chachu Ganya aliyepata kura 28,279.

9. Kaunti ya Kirinyaga

Ann Waiguru wa UDA amechaguliwa tena baada ya kupata kura 113,088 baada ya kumshinda Wangui Purity aliyekuwa na kura 105,677.

10. Kaunti ya Meru

Kawira Mwangaza ameshinda kiti hicho kwa tiketi ya kujitegemea. Amemshinda kiongozi wa sasa Kiraitu Murungi.

11. Kaunti ya Vihiga

Wilber Ottichilo wa Chama cha ODM amehifadhi kiti chake kwa kura 82,313.

Aliyekuwa gavana Moses Akaranga aliibuka wa pili kwa kura 42,432

12. Kaunti ya Homa Bay

Gladys Wanga wa ODM alishinda baada ya kupata kura 244,559. Evans Kidero aliibuka wa pili kwa kura 154,182.

13. Kaunti ya Nyamira

Mgombea wa chama cha United Progressive Alliance Amos Nyaribo amechaguliwa tena kuwa Gavana wa Kaunti ya Nyamira baada ya kupata kura 82,090.

Mpinzani wake wa karibu Walter Nyambati wa UDA alipata kura 49,281.

14. Kaunti ya Kisumu

Anyang’ Nyong’o wa ODM ameshinda kiti chake baada ya kupata kura 319,957.

Wa pili katika kinyang’anyiro hicho alikuwa Jack Ranguma wa NDG aliyepata kura 100,600

15. Kaunti ya Uasin Gishu

Jonathan Chelilim Bii maarufu Koti Moja amenyakua kiti hicho kwa kura 214,036.

Mgombea huru Zedekia Bundotich aliibuka wa pili kwa kura 127,013.

16. Kaunti ya Nakuru

Susan Kihika chini ya Chama cha UDA amechaguliwa kuwa Gavana baada ya kushinda kwa kura 440,707 na kumshinda Lee Kinyanjui 325,623.

17. Kaunti ya Bomet

Hilary Barchok amechaguliwa tena kuwa Gavana baada ya kushinda kwa kura 158,798 akimshinda mpinzani wake mkuu Isaac Rutto aliyepata kura 137,323.

Kaunti ya NyeriMutahi Kahiga wa UDA ndiye gavana mteule baada ya kupata kura 213,373.

18. Kaunti ya Kisii

Mbunge anayeondoka wa Dagoreti Kaskazini Simba Arati wa ODM alinyakua kiti hicho kwa kura 270,928.

Aliwashinda washindani wake saba akiwemo Ezekiel Machogu wa UDA aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 82,104.

19. Kaunti ya Laikipia

Joshua Irungu wa UDA alishinda kiti hicho baada ya kupata kura 113,783.

Bosi wa Kaunti anayeondoka Ndiritu Muriithi wa Jubilee aliibuka wa pili kwa kura 48,563.

20. Kaunti ya Kwale

Fatuma Achani wa UDA alipata kura 59,674 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Hamadi Boga wa ODM aliyepata kura 53,972.

21. Kaunti ya Kilifi

Gideon Mungaro wa ODM amenyakua kiti hicho akimshinda mbunge anayeondoka wa Malindi Aisha Jumwa wa UDA.

Mungaro alipata kura 143,773 huku Jumwa akipata kura 65,893.

22. Kaunti ya Kitui

Julius Malobe wa Wiper ameshinda kiti hicho baada ya kupata kura 198,004.

David Musila aliibuka wa pili kwa kura 114,606.

23. Kaunti ya Nyeri

Mutahi Kahiga wa UDA ndiye gavana mteule baada ya kupata kura 213,373.

24. Elgeyo Marakwet

Naibu Gavana wa Elgeyo Marakwet Wisley Rotich ameshinda kinyang'anyiro cha ugavana baada ya kupata kura 147,705 kwa tiketi ya chama cha UDA, huku mshindani wake wa karibu zaidi, kiongozi wa National Vision Party (NVP) Anthony Chelimo akiibuka wa pili kwa kura 11,759.

25. Kaunti ya Wajir

Ahmed Abdullahi Jiir (aliyekuwa Gavana) wa ODM ameshinda baada ya kuzoa kura 35,533 na kuwashinda washindani wake wote akiwemo gavana aliye madarakani Mohammed Abdi Muhamud aliyepata kura 521 pekee.

26. Kaunti ya Bungoma

Spika wa zamani Kenneth Lusaka (FORD-Kenya), ambaye alikuwa Gavana wa kwanza wa Kaunti ya Bungoma aliibuka mshindi baada ya kuzoa kura 241,695 dhidi ya mpinzani wake mkuu Wycliffe Wangamati (DAP-K) aliyezoa kura 137,378.

27. Kaunti ya Embu

Cecily Mbarire wa Chama cha UDA ameshinda kiti cha ugavana wa Embu baada ya kupata kura 108,610.Lenny Kivuti wa Devolution Empowerment Party (DEP) aliibuka wa pili kwa kura 105,246.

Zaidi yanafuata...