Wavinya Ndeti atwaa kiti cha ugavana Machakos

Ndeti ambaye alijaribu bila mafanikio 2013 na 2017 alishinda kiti hicho kwa kishindo

Muhtasari

•Ndeti alipata kura 226, 609 katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na mvutano mkali na kuwavutia wagombeaji watano.

•Seneta wa sasa wa Machakos Agnes Kavindu alihifadhi kiti chake baada ya kupata kura 155, 883.

Gavana wa Machakos amemteua Wavinya Ndeti akiwa na seneta Agnes Kavindu na mwakilishi wa wanawake Joyce Kamene, wote ambao walihifadhi viti vyao katika shule ya Machakos Academy, kituo cha kuhesabia kura kaunti hiyo Jumamosi, Agosti 13, 2022.
Gavana wa Machakos amemteua Wavinya Ndeti akiwa na seneta Agnes Kavindu na mwakilishi wa wanawake Joyce Kamene, wote ambao walihifadhi viti vyao katika shule ya Machakos Academy, kituo cha kuhesabia kura kaunti hiyo Jumamosi, Agosti 13, 2022.
Image: GEORGE OWITI

Mgombea ugavana wa Wiper Machakos Wavinya Ndeti ametangazwa mshindi baada ya kuwania nafasi hiyo mara mbili bila kufaulu.

Ndeti alipata kura 226, 609 katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na mvutano mkali na kuwavutia wagombeaji watano.

Msimamizi wa uchaguzi wa Kaunti ya Machakos Nelly Illongo alimtangaza CAS huyo wa zamani kuwa gavana mteule katika Chuo cha Machakos, kituo cha kuhesabia kura hiyo mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia Jumamosi.

Ndeti ambaye alijaribu bila mafanikio 2013 na 2017 alishinda kiti hicho kwa kishindo. Mshindani wake wa karibu Nzioka Waita (CCU) alifanikiwa kupata kura 129,181.

Kaunti ya Machakos kulingana na IEBC ina wapiga kura 687,565 waliosajiliwa.

Illongo alisema wapiga kura 408,175 walishiriki katika uchaguzi wa Agosti 9.

Idadi ya wapiga kura waliojitokeza ilikuwa asilimia 59.37.

Francis Maliti aliyegombea kwa tiketi ya chama cha Maendeleo Chap Chap kabla ya kuachia ngazi kwa Ndeti alipata kura 9, 981.

Rose Mulwa wa chama cha ELP alipata kura 4, 424 huku Johnson Muthama wa UDA akiwa na kura 37, 980.

Seneta wa sasa wa Machakos Agnes Kavindu alihifadhi kiti chake baada ya kupata kura 155, 883.

Kulikuwa na idadi ya wapiga kura 409, 729 kwa kiti, idadi iliyotafsiriwa kuwa asilimia 60.28.

Albanus Ngengele (UDA) aliibuka wa pili baada ya kupata kura 65, 606. John Katuku wa PTP alikuwa na kura 33, 752, Charles Kilonzo (mgombea huru) 43, 962, Joel Mbaluka (UDA) 39, 183, huku Benard Mung'ata wa MCCP akipata kura 62, 587.

Mwakilishi wa wanawake wa Machakos Joyce Kamene alishikilia kiti chake baada ya kupata kura 253, 106.

Rita Ndunge (MCCP) alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 93,778.