Aliyekuwa CEC wa Kiambu Karungo wa Thang'wa ameshinda kiti cha useneta wa kaunti hiyo.
Thang’wa ambaye aliwania kwa tiketi ya UDA alinyakua kiti hicho baada ya kupata kura 579,411.
Alimshinda mshindani wake wa karibu George Maara wa Jubilee ambaye alipata kura 112,304.
Thang’wa sasa atamrithi Seneta wa sasa Kimani Wamatangi ambaye amechaguliwa kuwa gavana wa kaunti hiyo.
Alikabiliana na wagombea sita ambao waliidhinishwa na IEBC.