Raila ambwaga Ruto katika eneo bunge la Kisauni na Bonchari

IEBC ilisema eneo bunge hilo lilikuwa na wapiga kura 135,690 waliosajiliwa.

Muhtasari
  • Haya ni kwa mujibu wa matokeo ya urais yaliyoidhinishwa na IEBC
  • Kiongozi huyo wa ODM alipata kura 35,190 dhidi ya mpinzani wake William Ruto aliyepata kura 21,887
  • Kiongozi wa Chama cha Roots, Goerge Wajackoyah alikuwa na kura 451 huku David Waihiga Mwaure wa Agano Party akipata kura 125
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Old Kibera mnamo Agosti 9, 2022.
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Old Kibera mnamo Agosti 9, 2022.
Image: THE STAR//ENOS TECHE

Mgombea urais wa Azimio Raila Odinga amepata kura nyingi katika eneo bunge la Kisauni kaunti ya Mombasa.

Haya ni kwa mujibu wa matokeo ya urais yaliyoidhinishwa na IEBC.

Kiongozi huyo wa ODM alipata kura 35,190 dhidi ya mpinzani wake William Ruto aliyepata kura 21,887.

Kiongozi wa Chama cha Roots, Goerge Wajackoyah alikuwa na kura 451 huku David Waihiga Mwaure wa Agano Party akipata kura 125.

IEBC ilisema eneo bunge hilo lilikuwa na wapiga kura 135,690 waliosajiliwa.

Kura halali zilikuwa 57,643 huku kura zilizokataliwa ni 572.

Katika eneo bunge la Bonchari Raila aliongoza kwa kura 29,198 huku mgombea urais wake wa UDA William Ruto akipata 12,706.

George Wajackoyah wa Roots alipata kura 165 akifuatiwa na David Mwaure aliyepata kura 81.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ilisema eneo bunge hilo lilikuwa na wapiga kura 64,630 waliojiandikisha, kura halali 42,150 na kura 484 zilizokataliwa.