Ruto ashinda katika eneo bunge la Kesses

IEBC ina siku saba baada ya siku ya uchaguzi kumtangaza rais mteule.

Muhtasari
  • Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ilisema eneo bunge hilo lilikuwa na wapiga kura 77,992 waliojiandikisha, kura halali 54,768 na kura 334 zilizokataliwa
Naibu rais William Ruto na waumini baada ya ibada Karen
Naibu rais William Ruto na waumini baada ya ibada Karen
Image: Facebook//WILLIAM RUTO

Naibu Rais William Ruto ameshinda eneo bunge la Kesses katika uthibitishaji unaoendelea wa kura za urais.

DP alipata kura 45,653 dhidi ya Raila Odinga wa Azimio aliyepata kura 8,966.

George Wajackoyah wa chama cha Roots alipata kura 88 huku chama cha Agano David Mwaure akipata kura 61.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ilisema eneo bunge hilo lilikuwa na wapiga kura 77,992 waliojiandikisha, kura halali 54,768 na kura 334 zilizokataliwa.

IEBC ina siku saba baada ya siku ya uchaguzi kumtangaza rais mteule.