Ruto Kifua mbele katika matokeo ya hivi punde huku matokeo rasmi ya IEBC yakizidi kuchelewa

Idadi hiyo inaonyesha kuwa Ruto ameshinda maeneo bunge 126 kwa kura 7,152,655 huku Raila akichukua maeneo bunge 146 akiwa na kura 6,942,708

Muhtasari

• Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa Ruto ndiye anayeongoza Raila kwa 52% ya kura

Matokeo ya uchaguzi wa urai kulingana na Radio Africa ambayo bado hayadhibitishwa na IEBC
Matokeo ya uchaguzi wa urai kulingana na Radio Africa ambayo bado hayadhibitishwa na IEBC
Image: THE STAR

Kucheleweshwa kwa muda mrefu kwa IEBC kutangaza matokeo ya mwisho yaliyoidhinishwa ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 kumeanza kusababisha sintofahamu. Kumekuwa na ripoti zinazokinzana kuhusu hali ya hesabu ya kura.

Fomu 34B ambazo zilizokuwa zimedhibitishwa na IEBC zinaonesha kwamba William Ruto anamwongoza Raila Odinga. Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa Ruto ndiye anayeongoza Raila kwa 52% ya kura katika jumla ya kura zilizokaribia kukamilika za fomu 34A.

Hesabu ya Radio Africa ya fomu 34B zote (ya muda na ambayo bado haijathibitishwa kikamilifu na IEBC) inaonyesha kuwa Ruto alipata asilimia 50.36 ya kura ikilinganishwa na asilimia 48.88 ya Raila.

Idadi hiyo inaonyesha kuwa Ruto ameshinda maeneo bunge 126 kwa kura 7,152,655 huku Raila akichukua maeneo bunge 146 akiwa na kura 6,942,708 huku maeneo bunge 18 yakisubiri (bila ya diaspora na magereza) - tofauti ya kura 209,947.

Hesabu ya kura inapatikana katika https://elections.thestar.ke na kuunganisha Fomu 34B zilizojumlishwa kwa maeneo bunge 291 na hesabu ya muda ya kitaifa. Radio Africa inasasisha hesabu ya mwisho ya vituo 49 vilivyosalia na kura 34, 815 ambazo zimesalia. Hata hivyo IEBC bado haijathibitisha na kutoa rasmi fomu zote za 34B kwa hivyo takwimu hizo zinafaa kushughulikiwa kwa tahadhari.