logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wetangula avuna ushindi mkubwa Bungoma

Seneta wa Bungoma Moses Wetang'ula amechaguliwa tena.

image
na SAMUEL MAINA

Uchaguzi14 August 2022 - 02:22

Muhtasari


  • •Matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka yalionyesha kuwa bosi wa Ford Kenya alipata kura 286,143.
  • •Machacha hadi sasa amekubali kushindwa na kuwashukuru, hasa watu wa Sirisia, ambao alisema walisimama naye.
Moses Wetangula

Seneta wa Bungoma Moses Wetang'ula amechaguliwa tena.

Matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka yalionyesha kuwa bosi wa Ford Kenya alipata kura 286,143.

Chama cha Ford-Kenya kinachoongozwa na Wetangula ni mshirika katika muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Naibu Rais William Ruto.

Naibu gavana wa Bungoma anayeondoka Charles Ngome, mwanahabari Advice Mundalo na mwanasiasa Machacha Machembe walikuwa wametupa kofia zao ulingoni kwa nia ya kumtimua Wetangula.

Machacha hadi sasa amekubali kushindwa na kuwashukuru, hasa watu wa Sirisia, ambao alisema walisimama naye.

"Nataka kuwashukuru wote waliosimama nami na kunipigia kura, hasa Sirisia, ambako nilipata kura 21,000," Machacha alisema.

Mnamo Agosti 10, Machacha alimsifu Wetangula kwa ushindi mkubwa wa kuhifadhi kiti chake.

"Kulingana na matokeo ya awali yanayotiririka, inaonyesha kuwa Wetang'ula anachukua kiti hiki mapema sana," alisema.

"Uchaguzi sio wa kupigana, wacha washiriki wengine katika nyadhifa zingine wakubali matokeo ya kura na waunge mkono wale walioshinda."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved