(+Picha) Ruto awasili Bomas ambako matokeo ya urais yanatarajiwa kutangazwa

Msafara wa Ruto uliwasili Bomas mwendo wa saa tisa kasorobo.

Muhtasari

•Ruto amewasili katika kituo cha kitaifa cha kujumuisha kura cha   Bomas of Kenya kabla ya matokeo ya urais kutangazwa na IEBC.

•Chebukati katika taarifa yake alisema tume ya uchaguzi na mipaka itamtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Jumatatu saa tisa alasiri.

awasili katika Bomas of Kenya kabla ya matokeo ya urais kutangazwa mnamo Agosti 15, 2022.
Naibu rais William Ruto awasili katika Bomas of Kenya kabla ya matokeo ya urais kutangazwa mnamo Agosti 15, 2022.
Image: DOUGLAS OKIDY

Naibu Rais William Ruto amewasili katika kituo cha kitaifa cha kujumuisha kura cha   Bomas of Kenya kabla ya matokeo ya urais kutangazwa na IEBC.

Msafara wa Ruto uliwasili Bomas mwendo wa saa tisa kasorobo.

Mgombea urais huyo wa Kenya Kwanza alikuwa ameandamana na baadhi ya wanachama wengine wa muungano huo.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati katika barua kwa vyombo vya habari alisema tume ya uchaguzi na mipaka itamtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Jumatatu saa tisa alasiri.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inakualika kuangazia tangazo la Matokeo ya Urais mnamo Jumatatu Agosti 15, 2022 katika Bomas of Kenta saa tisa alasiri," Barua iliyoachiwa na IEBC ilisoma.

Naibu rais awasili katika ukumbi wa Bomas kabla ya matangazo ya urais kutolewa mnamo Agosti 15, 2022.
Naibu rais awasili katika ukumbi wa Bomas kabla ya matangazo ya urais kutolewa mnamo Agosti 15, 2022.
Image: DOUGLAS OKIDY

Chebukati anatarajiwa kumtangaza rais mpya wa Kenya baada ya shughuli ya uhakiki wa fomu za matokeo ya urais kutoka maeneobunge yote na ujumuishaji wa kura  kukamilika.

Uhakiki wa fomu za matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9  ulikamilika Jumatatu asubuhi baada ya kuendelezwa kwa siku tano.

Hapo awali, kiongozi wa Roots Party George Wajackoyah na David Mwaure wa Agano walifika katika ukumbi wa Bomas of Kenya kabla ya kutangazwa rasmi kwa matokeo.

Kwa sasa, kwaya ya kikatoliki inawaburudisha wanasiasa na waalikwa wengine katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura.

Siku ya Jumapili, wagombeaji wawili wakuu wa urais- Raila Odinga na Ruto- walihudhuria ibada tofauti za kanisa huko Karen na kuwataka wafuasi wao kudumisha utulivu na uvumilivu hata wasiwasi kuhusu kura ukizidi kupamba moto.