logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto ang'aa nyumbani kwa Mudavadi

Ruto alipata kura 22,087 huku Raila akiwa na kura 19,743.

image
na Samuel Maina

Uchaguzi15 August 2022 - 04:12

Muhtasari


  • •Sabatia ni nyumbani kwa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, ambaye alimtema Raila Odinga na kujiunga na Ruto kwenye Kenya Kwanza.

Mgombea urais wa UDA William Ruto alipata kura nyingi zaidi katika eneo bunge la Sabatia, kaunti ya Vihiga.

Sabatia ni nyumbani kwa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, ambaye alimtema Raila Odinga na kujiunga na Ruto kwenye Kenya Kwanza.

Ruto alipata kura 22,087 huku Raila akiwa na kura 19,743.

Wagombea urais George Wajackoyah wa chama cha Roots na David Mwaure w a Agano walipata kura 330 na 126 mtawalia.

Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura katika eneo bunge hilo ilikuwa 70,875.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema kura 42,286 kati ya zilizopigwa zilikuwa halali.

Idadi ya kura zilizokataliwa ilikuwa 343.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved