logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Makamishna 4 wa IEBC waliopinga matokeo kutoa taarifa

Wanne hao watatoa hotuba yao Jumanne alasiri katika hoteli ya Serena.

image
na Samuel Maina

Uchaguzi16 August 2022 - 12:04

Muhtasari


  • •Wanne hao wakiongozwa na naibu mwenyekiti Juliana Cherera watatoa hotuba yao Jumanne alasiri katika hoteli ya Serena.
  • •Jumatatu jioni makamishna hao walijitenga na matokeo ya uchaguzi wa urais hata kabla ya kutangazwa na mwenyekiti Wafula Chebukati
Makamishna Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyangaya.

Makamishna wanne wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini ambao walijitenga na matokeo ya urais wanatarajiwa kuhutubia wanahabari.

Wanne hao wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa tume Juliana Cherera watatoa hotuba yao Jumanne alasiri katika hoteli ya Serena, jijini Nairobi.

Pamoja na Cherera ni makamishaa; Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyangaya ambao wote waliteuliwa rais Uhuru Kenyatta mwaka jana.

Jumatatu jioni makamishna hao walijitenga na matokeo ya uchaguzi wa urais hata kabla ya kutangazwa na mwenyekiti Wafula Chebukati

Walifanya mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli hiyo hiyo ya Serena na kueleza kutoridhishwa kwao na jinsi hatua ya mwisho ya uchaguzi ilivyoendelezwa.

"Tumefanya uchaguzi wa 2022 kwa njia bora zaidi. Tumehakikisha kuwa tumeboresha viwango.  Tumefanya kazi nzuri lakini baadhi ya mambo yanahitaji kuwekwa wazi.Tupo hapa kwa sababu ya hali ya kutoeleweka ambayo hatua ya mwisho ya uchaguzi mkuu huu. Hatuwezi kuchukua umiliki wa matokeo ambayo yanaenda kutangazwa," Cherera alisema.

Naibu mwenyekiti huyo wa IEBC alibainisha kuwa watu ambao hawataridhishwa na matokeo wapo huru kuelekea mahakamani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved