Polisi wakabiliana na vijana huku ghasia zikishuhudiwa Kisumu

Wakazi hao walikabiliana na polisi katika mapigano ya paka na panya.

Muhtasari

• Maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia walilazimika kupiga vitoa machozi kuwatawanya vijana.

Ghasia zimezuka Kondele mjini Kisumu baada ya Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kumtangaza Naibu Rais William Ruto kuwa Rais mteule mnamo Agosti 15, 2022. Picha: DANIEL OGENDO
Ghasia zimezuka Kondele mjini Kisumu baada ya Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kumtangaza Naibu Rais William Ruto kuwa Rais mteule mnamo Agosti 15, 2022. Picha: DANIEL OGENDO

Ghasia zilizuka katika eneo la Kondele mjini Kisumu baada ya Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kumtangaza William Ruto kuwa Rais Mteule Jumatatu Agosti 15, 2022.

Machafuko ya ghafla yalizuka mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais.

Wakazi hao walikabiliana na polisi katika mapigano ya paka na panya.

Picha: DANIEL OGENDO
Picha: DANIEL OGENDO
Raia anaonekana kwenye baiskeli. Ghasia zimezuka Kondele mjini Kisumu baada ya Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kumtangaza Naibu Rais William Ruto kuwa Rais mteule mnamo Agosti 15, 2022. Picha: DANIEL OGENDO

Jumatatu kuanzia saa tisa alasiri, dalili za vurumai zilitanda katika mzunguko wa Kondele.

Maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia walilazimika kupiga vitoa machozi, na kuwalazimu vijana waliokuwa wamejazana eneo hilo kukimbilia usalama wao.