Wafahamu makamishna wa tume ya IEBC baada ya mgawanyiko kuhusu matokeo

Katibu wa Mkakati wa Kufufua Uchumi na Urithi wa Kaunti ya Mombasa.

Muhtasari

• Makamishna wanne wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka  wakiongozwa na makamu mwenyekiti Juliana Cherera, walisema hawakuhusika na uamuzi

Muda mfupi tu kabla ya  William Ruto  kutangazwa kama rais mteule,palitokea jambo ambalo liliishtua nchi siku ya Jumatatu.Makamishna wanne wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka  wakiongozwa na makamu mwenyekiti Juliana Cherera, walisema hawakuhusika na uamuzi wa matokeo ya mwisho yaliyokuwa yakitangazwa na mwenyekiti wao Wafula Chebukati .

Tume hiyo ina makamishna saba tu.

Tangazo la kundi hilo lililojitenga limeongeza wasiwasi nchini humo.

Sheria ya uchaguzi hata hivyo inampa mwenyekiti jukumu la kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais na Chebukati aliendelea kutekeleza jukumu hilo na kumtangaza

Je,makamishna wa IEBC  ni akina nani?

Wafula Chebukati-Mwenyekiti

Image: GETTY IMAGES

Wafula Chebukati ,mwanasheria ndiye mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) inayohusika na mchakato mzima wa uchaguzi nchini Kenya.Ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi wa urais ambaye leo amemtangaza naibu wa rais William Ruto kama rais mteule wa Kenya baada ya kushinda uchaguzi

 Ana zaidi ya miaka 36 ya uzoefu katika tasnia ya sheria.

 Anafanya kazi kwa wakati wote kama Mwenyekiti wa Tume

 Rais wa Baraza Kuu la Muungano wa Mamlaka za Uchaguzi Afrika.

 Uanachama:

            - Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK)

           - Taasisi ya Makatibu Walioidhinishwa (ICS)

           - Tume ya Kimataifa ya Wanasheria (ICJ) -Kenya

 

Juliana Cherera-Makamu Mwenyekiti

Bi Cherera ni naibu mwenyekiti wa tume ya  IEBC  na ndiye aliyewaongoza  makamishna wengine watatu kujitenga na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati  yaliyompa ushindi William Ruto kama rais mteule.

Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 18 katika Elimu na Usimamizi katika sekta ya umma.

Kabla ya uteuzi wake katika Tume, alifanya kazi kama Afisa Mkuu Mtendaji katika Kitengo cha Utoaji Mkakati wa Serikali ya Kaunti ya Mombasa.

Mwanachama wa Kamati ya Kuratibu Miradi ya Kusaidia familia  na Kusaidia Lishe katika Kaunti ya Mombasa.

Katibu wa Mkakati wa Kufufua Uchumi na Urithi wa Kaunti ya Mombasa.

Mwanachama wa Kamati ya Mpango wa Usaidizi wa Ugatuzi nchini Kenya.

Anafanya kazi kwa muda wote kama makamu mwenyekiti wa Tume.

Ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ya Mpiga Kura, Ushirikiano na Wadau.

Bw. Francis Wanderi-Kamishna

Ana zaidi ya miaka 32 katika usimamizi mkuu ndani ya taasisi za umma na za kibinafsi zilizo na sifa ya uadilifu na utendaji wa juu, na rekodi iliyothibitishwa katika maendeleo na utekelezaji wa mkakati, watu na usimamizi wa mabadiliko na, uongozi na uvumbuzi kuelekea utekelezaji wa malengo na maono ya shirika.

Ni mmoja wa makamishna ambao wamejitenga na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti Wafula Chebukati .

Francis M. Wanderi ni Mwenyekiti wa zamani wa EPZ na mkurugenzi Roots Credit Ltd.

Anaongoza Kamati ya Usimamizi wa Fedha na Ugavi

  Bw. Justus Nyang'aya-Kamishna

Makamishna wanne wa IEBC waliojitenga na matokeo ya uchaguzi wa urais
Makamishna wanne wa IEBC waliojitenga na matokeo ya uchaguzi wa urais

Nyang’aya ana uzoefu wa zaidi ya miaka 32 katika Uongozi wa Kimkakati, Utawala Bora na Mashirika ya Uwajibikaji kwa Jamii.

Alikuwa mkurugenzi wa Lead Africa, shirika linalofanya kazi kwa kufuzu kwa Wasimamizi wa Kiafrika.Ni miongoni mwa waliojitenga na matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyofanywa na mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati .

Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Nchi, Amnesty International Kenya. Kazi ya Amnesty Kenya inajikita zaidi katika kuzuia kufukuzwa kwa lazima, ulinzi wa haki za makazi na haki za wanawake.

Pia alifanya kazi katika Shirika la Maendeleo la Uholanzi pamoja na UNESCO.

Anaongoza Kamati ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

  Irene Masit-Kamishna

Irene Masit ana uzoefu wa kazi na maarifa zaidi ya miaka 25 katika Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Yeye ni mjumbe wa zamani wa bodi, Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Eneo Bunge la Serikali (NGCDF). Ni miongoni mwa makamishna waliojitenga na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati .

Ana ujuzi na uzoefu katika Fedha, Utawala, Usimamizi na Utawala wa Umma.

Anaongoza Kamati ya Sheria, Uzingatiaji na Uhusiano wa Vyama vya Siasa na Kamati ya Uongozi na Uadilifu.

Prof. Abdi Yakub Guliye-Kamishna

Guliye ana zaidi ya miaka 27 ya tajriba ya kufundisha chuo kikuu, ambapo katika miaka 7 iliyopita alikuwa na majukumu ya ziada ya utawala/usimamizi.

Pia alihudumu katika Bodi mbalimbali za Taasisi/Mashirika, akiwa na kamati zenye uenyekiti kama vile Ukaguzi na Usimamizi wa Vihatarishi pamoja na Fedha.

Anaongoza Kamati ya Uendeshaji, Utafiti na Uwekaji Mipaka ya Uchaguzi.

Bw.Boya Molu-Kamishna

Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika Usimamizi wa Rasilimali Watu na utawala haswa katika sekta ya umma.

Kabla ya kujiunga na Tume Bw. Molu alihudumu katika nyadhifa mbalimbali katika Benki Kuu ya Kenya (CBK) na Idara ya Mahakama katika Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala.

Pia aliwahi kuwa mjumbe wa baraza la Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (IHRM) Kenya.

 Anasimamia  Kamati ya Rasilimali Watu, Utawala na Mafunzo.