Makau Mutua azungumza kuhusu kushindwa kwa Raila Odinga katika uchaguzi

Kundi ya Azimio sasa wako na matumaini ya kusikilizwa katika mahakama ya juu

Muhtasari

•Odinga alipinga matokeo hayo, na kusema atawasilisha kesi katika Mahakama ya Juu ya Kenya.

•Hii ni baada ya ushindi wa William Ruto katika uchaguzi wa urais kuleta mgawanyiko ndani ya tume hiyo ya IEBC.

Makau Mutua
Makau Mutua

Msimamizi wa kamati wa kampeni wa urais ya Azimio la Umoja one Kenya Makau Mutua, hatimaye alisema kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alifaa kuafikiana na wenzake  kabla ya kutoa matokeo ya kura za urais Jumatatu.

Hii ni baada ya ushindi wa William Ruto katika uchaguzi wa urais kuleta mgawanyiko ndani ya tume hiyo.

Makamishna wanne wa IEBC, akiwemo naibu mwenyekiti Juliana Cherera, walisema "Hawangeweza kumiliki" matokeo kwa sababu Chebukati alikuwa amewatenga wakati wa hatua za mwisho za kujumlisha kura.

Matokeo yaliyotolewa hatimaye na Chebukati yalionyesha kuwa Ruto alipata kura milioni 7.18 (asilimia 50.49) dhidi ya 6.94 milioni za  Raila Odinga (asilimia 48.85).

Odinga alipinga matokeo hayo, na kusema atawasilisha kesi katika Mahakama ya Juu ya Kenya.

Kinara huyo wa Azimio Raila Odinga amekusanya kundi la mawakili wenye uwezo mkubwa katika kesi ya kupinga ushindi wa William Ruto.

Ni mawakili wakuu, wanasheria wenye uzoefu na mawakili wengine wenye ujuzi wa kuandaa na kuunda hoja za kisheria.

Baadhi ya mawakili hao walikuwa katika kesi ya 2017 ambapo Mahakama ya Juu ilibatilisha uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Mahakama hiyo, iliyoongozwa na Jaji Mkuu David Maraga, ilibatili uchaguzi huo baada ya kubaini ulikumbwa na ukiukwaji wa sheria na kasoro.

Kundi hiyo ya Azimio one Kenya, sasa wako na matumaini kuwa Jaji mkuu wa sasa Martha Koome pia watawasikiliza  na kufanya uamuzi mwafaka kuhusu uchaguzi uliopita.