Baadhi ya Matakwa ya Azimio waliyowasilisha katika mahakama ya upeo wa juu

Wanataka mahakama pia kuwasikiliza makamishna 4 waliojitenga na matokeo hayo.

Muhtasari

• Azimio wanaitaka mahakama kumshrutisha Ruto na tume ya IEBC kulipia gharama ya kesi hiyo.

Wakiwasilisha faili za maombi yao katika mahakama ya upeo
Viongozi wa Azimio Wakiwasilisha faili za maombi yao katika mahakama ya upeo
Image: Maktaba

Mpeperusha bendera wa Muuungano wa Azimio la Umoja One Kenya Jumatatu adhuhuri aliwasili katika mahakama ya Milimani kwa kishindo huku akiwa ameandamana na wakereketwa wa muungano huo pamoja na makumi ya mawakili bila kusahau lori zima lililokuwa limesheheni nakala za maombi ambayo anaitaka mahakama ya upeo kuzingatia.

Haya hap ani baadhi ya maombi hayo;

  1. Odinga na Azimio wanaitaka tume ya IEBC na mwenyekiti wake, Chebukati kuwakabidhi stakabadhi na vifaa vya uchaguzi chini ya saa 48.
  2. Tume ya IEBC na mwenyekiti Wafula Chebukati kuruhusu ukaguzi wa mitandao iliyotumiwa kuhifadhi nyaraka za matokeo ya urais katika muda huo huo was aa 48.
  3. Muungano huo pia unaitaka mahakama kuishrutisha idara ya DCI kuwasilisha vifaa na stakabadhi zilizopatikana mikononi mwa raia wa Venezuela pamoja na tarakilishi za ajenti wa chama cha UDA na matokeo yake.
  4. Wanataka ukaguzi wa kura zote zilizoharibika na zile zilizokataliwa kwani kulingana nao kura hizo ni muhimu katika kutathmini matokeo ya urais haswa katika asilimia.
  5. Ukaguzi wa kina wa fomu 34A, 34B na 34C
  6. Ukaguzi wa kina wa mitambo ya kidijitali ya KIEMS na hifadhi ya matokeo kwenye tovuti ya tume ya IEBC.
  7. Odinga na kambi yake wanaitaka mahakama kutoa hakikisho kwamba iwapo ushindi wa Ruto utatupiiwa mbali basi IEBC kuhesabu upya na kukagua matokeo ya kura hizo za urais na kuwatangaza Raila na Karua kama rais na naibu wake mtawalia.
  8. Kuwa IEBC ilivyo sasa, haiwezi kuandaa uchaguzi ulio huru na haki
  9. Azimio wanadai kuwa mahakama inafaa itambue Kuwa kulikuwa na dosari nyingi zilizoathiri matokeo ya urais
  10. wanaitaka mahakama kuhakikisha kwamba Kura zisizo halali zimeondolewe katika matokeo ya mwisho ya urais
  11. Mahakama iamuru Kuwa matokeo sio halali kwa mujibu wa sheria
  12. Mahakama ya upeo idhibitishe Kuwa Ruto hakufikia hitaji la katiba la 50%+1 ya kura zilizopigwa na kutangazwa kwake kulikuwa kinyume na sheria
  13. Azimio wanataka mahakama kuharamisha Cheti na chapisho la Ruto kuwa mshindi kwenye gazeti rasmi la serikali.
  14. IEBC iandae uchaguzi mwingine wa urais kwa mujibu wa sheria iwapo dosari hizo wanazozitaja zitabainika na majaji.
  15. Wanadai kwamba Tangazo la makamishna 4 kupinga matokeo litambuliwe na kusikilizwa mahakamani.
  16. Uamuzi wa washtakiwa 1,2,3,4,9 ulikiuka kanuni za uchaguzi
  17. Wanataka mahakama iamuru kwamba mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hafai kushikilia afisi ya umma kwa kile wanakitaja kuwa amehujumu maadili na imani ya umma katika IEBC
  18. Azimio wanataka tume ya IEBC, mwenyekiti wake Wafula Chebukati na naibu rais anayeondoka Ruto kulipia gharama ya kesi hiyo.