logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gladys Wanga atoa tahadhari kwa wafanyikazi wa kaunti ya Homa Bay

''Kuna wale watu ambao wanajiita Cartels, usipochunga utajipata mahali pabaya,utalaghaiwa na kulipa fidia zisizo za haki, ukitaka kufanya biashara na kaunti fuata sheria'' Gladys Wanga alieleza.

image
na Davis Ojiambo

Uchaguzi23 August 2022 - 08:56

Muhtasari


  • •Mwanasiasa huyo alidokeza kuwa kuna wafanyikazi wa kaunti hiyo ambao waliajiriwa kupitia mlango wa nyuma kinyume na sheria.
  • •Gavana mteule huyo na naibu wake wanatazamiwa kuapishwa wiki hii katika uga wa Homa Bay, ambao watu wengi kutoka kaunti hiyo watahudhuria hafla hiyo.

Gavana mteule wa Homa Bay kaunti Gladys Wanga, sasa ametoa ilani kwa wafanyikazi wa kaunti hiyo akisema kuwa atakapoapishwa rasmi na mgombea mweza wake Joseph Oyugi Magwanga, watahakikisha kuwa maswala ya ufisadi wamepambana nayo.

Mwanasiasa huyo alidokeza kuwa kuna wafanyikazi wa kaunti hiyo ambao waliajiriwa kupitia mlango wa nyuma kinyume na sheria.

''Tunapojiandaa kuapishwa, jukumu letu kubwa itakuwa kuchuguza jinsi wafanyikazi wengine walijipata katika baadhi za ofisi za kaunti,kwasababu kuna tetezi kwamba wengine waliajiriwa kutozingatia sheria'' Gladys alisema.

Aliongeze kwa  kutahadharisha umma kuwa makini na kutembelea ofisi husika wakati wanapotafuta kandarazi kwa hiyo kaunti.

''Kuna wale watu ambao wanajiita Cartels, usipochunga utajipata mahali pabaya,utalaghaiwa na kulipa fidia zisizo za haki, ukitaka kufanya biashara na kaunti fuata sheria'' Gladys Wanga alieleza.

Hata hivyo gavana huyo mteule alisisitiza kuwa  kwa sasa hawatashughulika na uajiri wa wafanyikazi, kwani lazima wajadiliane kwanza kuhusu nafasi zilioko na kutangaza rasmi nafasi hizo.

Gladys Wanga aligombea kiti hicho kwa tiketi  ya ODM na kubwaga mpizani wake wa karibu aliyekuwa gavana wa Nairobi Evance Kidero.

Baada ya kuaapishwa rasmi, atakuwa gavana wa pili wa kaunti hiyo, akichukua wadhifa huo kutoka kwa Cyprian Awiti ambaye ni gavana anayeondoka mamlakani.

Gavana mteule huyo na naibu wake wanatazamiwa kuapishwa wiki hii katika uga wa Hom Bay ambao watu wengi kutoka kaunti hiyo watahudhuria hafla hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved