logo

NOW ON AIR

Listen in Live

IEBC yachapisha majina ya wabunge 286 kwenye gazeti la Serikali

“IEBC inatangaza kwamba watu ambao majina yao yameorodheshwa katika ratiba iliyo hapa chini walichaguliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Kitaifa baada ya kupata kura nyingi zilizopigwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 9 Agosti, 2022 na kutii masharti ya Sheria ya Uchaguzi, 2011 na Katiba,” notisi hiyo ilidokeza.

image
na Radio Jambo

Habari23 August 2022 - 13:18

Muhtasari


•Notisi hiyo imechapisha wanachama 286 waliochaguliwa na majina yao pamoja na idadi ya kura walizopata katika uchaguzi iliyopita.

•Kioko alidokeza kuwa Wabunge Wateule watafahamishwa mara tu Rais Uhuru Kenyatta atakapotangaza tarehe watakayokutana kwa kikao cha kwanza.

bungeni

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetangaza kwenye gazeti la serikali Wabunge Wateule kutoka maeneo bunge 286.

Chapisho hiyo haijajumuisha  maeneo bunge manne ambapo uchaguzi umepangwa kufanyika Jumatatu wiki ijayo, ikiwa ni pamoja na Kitui vijijini, Rongai, Kacheliba na Pokot kusini.

Notisi ya Gazeti la Serikali imechapishwa kabla ya wabunge hao kuwa na kongamano ya maelekezi hapo Alhamisi itakayo fanyika katika majengo ya Bunge.

Notisi hiyo imechapisha wanachama 286 waliochaguliwa na majina yao pamoja na idadi ya kura walizopata katika uchaguzi iliyopita.

“IEBC inatangaza kwamba watu ambao majina yao yameorodheshwa katika ratiba iliyo hapa chini walichaguliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Kitaifa baada ya kupata kura nyingi zilizopigwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 9 Agosti, 2022 na kutii masharti ya Sheria ya Uchaguzi, 2011 na Katiba,” notisi hiyo ilidokeza.

Karani wa Bunge la Kitaifa Serah Kioko mnamo Ijumaa aliwahimiza wabunge wote waliochaguliwa ikiwa ni pamoja na wanachama ambao wamechaguliwa tena kujitokeza kwa ajili ya kikao cha mwelekeo.

Kioko alisema kuwa vikao elekezi vitajumuisha usajili wa Wajumbe, ukusanyaji wa taarifa za bio-data, utoaji wa vitambulisho vya ubunge, kutoa taarifa ya matumizi ya mfumo wa upigaji kura wa Chemba.

Alisema pia kuwa itahusisha pia ziara ya Majengo ya Bunge na maelezo mafupi ya Ofisi ya Karani juu ya mambo muhimu ya kisheria, kati ya mambo mengine.

Kioko alidokeza kuwa Wabunge Wateule watafahamishwa mara tu Rais Uhuru Kenyatta atakapotangaza tarehe watakayokutana kwa kikao cha kwanza.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved