logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nicholas Gumbo afanya mkutano na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi

Alipokelewa na Kiongozi huyo wa ANC ambaye pia ni mmoja wa viongozi katika muungano wa Kenya Kwanza.

image
na Davis Ojiambo

Uchaguzi23 August 2022 - 12:56

Muhtasari


  • •Kwa uchaguzi uliofanyika mnamo Agosti 9, Nicholas Gumbo alishindana na James Orengo kwa lengo ya kuwa gavana wa Siaya.
KiongozI wa ANC, mwanasiasa Gumbo na viongozi wengine

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amekutana na aliyekuwa mbunge wa zamani wa Rarieda Nicholas Gumbo.

Gumbo ambaye aliwania kiti cha gavana wa kaunti ya Siaya kwa tiketi ya chama cha UDM na kupoteza kwa Seneta James Orengo alikuwa ameandamana na gombea mwenza David Ohito kwa mkutano kwenye makao makuu ya chama cha ANC.

Duru zaarifu kuwa mkutano huo ulijadili mikakati ya mwanasiasa huyo kuungana na Muungano wa Kenya Kwanza. Chama chake cha UDM tayari kimetia saini mkataba wa ushirikiano na muungano wa Kenya Kwanza baada ya kutangaza kugura Azimio.

Alipokelewa na Kiongozi huyo wa ANC ambaye pia ni mmoja wa vinara wa Kenya Kwanza.

Gumbo aliwania kiti hicho cha ugavana wa Kaunti ya Siaya na kushindwa na seneta James Orengo wa ODM.

Mwanasiasa huyo alikuwa kiwania wadhifa huo kwa mara ya pili baada ya kukosa kufua dafu mwaka 2017.

Katika jaribio la kwanza alishindwa na Coronel Rasanga ambaye alikuwa akiwania kiti hicho kwa muhula wa pili.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved