Mutula Kilonzo azungumza kuhusu Kumbukumbu ya rais Uhuru

Mutula alisema kuwa rais anafaa kuwa mtulivu na si mtu mwenye wasi wasi

Muhtasari

•Rais Kenyatta alikutana na viongozi wa dini katika Ikulu, ambapo aliwahakikishia kuwa  shughuli za mpito ya serikali  utakuwa mwepesi.

Gavana mteule Mutula
Gavana mteule Mutula
Image: Hisani

Gavana mteule wa Makueni Mutula Kilonzo Junior amesema kumbukumbu  wa rais anayeondoka Uhuru Kenyatta utategemea pakubwa jinsi atakayomkabidhi mamlaka yule atakaye mfuata kama rais.

Katika mahojiano na moja ya vyombo vya habari, Mutula alisema rais Kenyatta anafaa kujitokeza na kuwahakikishia Wakenya kuhusu uridhi wa amani.

“Kama ningekuwa Uhuru ningetoka nje, tumwone juu ya gari lake. Na aonekane mwenye furaha, kana kwamba hana wasi wasi. Yeye ndiye rais anayeondoka na hakuna mtu ambaye angejiuliza Uhuru yuko wapi,” Mutula alisema.

Rais Kenyatta amekaa kimya kufuatia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 ambapo naibu wake William Ruto alishinda mgombea wa urais Raila Odinga ambaye alikuwa akiwania kupitia tiketi ya  Azimio La Umoja One Kenya.

Odinga na walalamishi wengine wanane walienda Mahakama ya Juu zaidi ili ushindi huo ufutiliwe mbali.

Rais Kenyatta alikutana na viongozi wa dini katika Ikulu, ambapo aliwahakikishia kuwa  shughuli za mpito huo  utakuwa mwepesi.

“Kuna wakati tulikuwa na mkutano kuhusu BBI na tulikuwa katika Ikulu na nilimwambia rais kwamba kumbukumbu wake mkubwa atakayoiacha sio BBI au barabara nzuri. Nilimwambia kwamba kumbukumbu wake mkubwa ni wakati atakapokabidhi mamlaka kwa amani,” Mutula

Mutula aliongeza kuwa  rais anafaa kuwa mtulivu na si mtu mwenye wasi wasi , na  pia kuhakikisha kuwa Kenya inazidi kudumisha amani.