IEBC yamjibu Raila kuhusu chaguzi za Mombasa na Kakamega

Muhtasari

•Uchaguzi hizo sasa zimepagwa kufanyanyika Agosti 29, hili maeneo hizo waweze kuapata magavana wao.

akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 10, 2022
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 10, 2022
Image: ENOS TECHE

Tume huru ya mipaka na uchaguzi (IEBC) kupitia  kupitia mtandao wa Twitter imepinga vikali pendekezo la kinara wa Azimio Raila Odinga ya kumfungia nje mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati dhidi ya kujihusisha na  chaguzi za ugavana za Kakamega na Mombasa.

Tume hiyo imesema kuwa kiongozi huyo hafai kupotosha umma kuhusu sheria za uchaguzi za humu nchini.

 

''Tume hii ingependa kufahamisha umma kuwa matamshi ya Raila huenda yakawapotosha watu wengi wakati huu ambao chaguzi za Kakamega na Mombasa zinatazamiwa kufanyika mno Agosti 29,'' tume hiyo ilichapisha katika ukurasa wake wa twitter

Tume ya IEBC iliahirisha chaguzi za Kakamega na Mombasa baada ya kugundua kwamba karatasi za kupigia kura zilikuwa na hitilafu.

Chaguzi hizo sasa zimepagwa kufanyanyika Agosti 29.

Kiongozi wa Azimio one Kenya Raila Odinga alitaka mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kujiondoa kwenye usimamizi wa chaguzi za Mombasa na Kakamega.

Raila ambaye siku ya Jumatato alikuwa katika kaunti ya Mombasa kumpigia debe mgombea wa ugavana wa Mombasa kwa tiketi ya ODM Abdullswamad Nassir, alisema kuwa tume hiyo inafaa kusimamiwa na  naibu mwenyekiti wake Julliana Cherera.

Mwanasiasa huyo alisema kuwa Chebukati anakabiliwa na kesi katika mahakama ya juu, kwa hivyo hawana imani naye kusimamia chaguzi zilizosalia ambazo zinafaa kufanyika Agosti 29.

''Alitangaza mpizani wetu mshindi katika uchaguzi wa urais uliopita  licha ya sisi kushinda uchaguzi huo, hatua ambayo maafisa wengine wa IEBC wakiongozwa na naibu wake Cherera hawakukubaliana nayo, sasa tunataka Naibu wake Cherera kusimamia chaguzi zilizosalia'' Raila alisema.

Kiongozi huyo aliwarai vijana pamoja na wanawake kujitokeza na kupigia kura kwa fujo  mgombea wa ODM.

''Hapa Mombasa ni ngome ya ODM, na wanaazimio wote, kwa hivyo lazima mjitokeze na kuonyesha kuwa nyinyi ni wafuasi wa baba  na kumpigia  NassirAbdullswamad Sheriff kura'' Raila alisema.

Nassir atakuwa akipambana na  Hassan Omar Sarai wa   (UDA),ambaye ni mpinzani wake wa karibu katika kinyanganyiro cha kuwa gavana wa kaunti ya Mombasa. 

Wote wawili sasa wako mbioni kuchukua hatamu ya uongozi kutoka kwa gavana anayeondoka Hassan Joho, ambaye amekuwa gavana wa kaunti hiyo kwa mihula miwili.

Raila Odinga pia aliwahakikishia wafuasi wake kuwa watashinda  kesi ambayo wamewasilisha katika mahakama ya juu ya upeo.

''Mawakili wetu walifanya kazi nzuri sana na kuandika chini yale malalamishi yetu kwa ufasaha, sasa ni jukumu la korti kuhakikisha kuwa haki imetendeka kwa Kenya,'' Raila alisema.