Lazima uende nyumbani-Sudi amwambia kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu

Sudi alidai kuwa kamishna huyo wa kaunti alipanda mbegu za mifarakano kabla ya uchaguzi wa Agosti 9, mwaka huu.

Muhtasari
  • Mbunge wa Kapseret Oscar amemwambia kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Stephen Kihara kujiandaa kwenda nyumbani
Mbunge Oscar Sudi
Image: Oscar Sudi/TWITTER

Mbunge wa Kapseret Oscar amemwambia kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Stephen Kihara kujiandaa kwenda nyumbani.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuapishwa kwa gavana Jonathan Bii, almaarufu Koti Moja, Sudi alidai kuwa kamishna huyo wa kaunti alipanda mbegu za mifarakano kabla ya uchaguzi wa Agosti 9, mwaka huu.

"Wewe county commissioner unajua ya kwamba ulitenganisha watu wetu hapa na fitina mingi. Sisi tumekusamehea but you must resign from this government. Hatuwezi kukubali hii maneno," Sudi alizungumza.

Mbunge hata hivyo hakutoa ushahidi wowote kuunga mkono dai lake.

Sudi aliendelea kudai kuwa kamishna wa kaunti alitaka kuzua vita katika eneo hilo, madai Star haikuweza kuthibitisha.

"Tuambiane ukweli ndop nchi ipone. Mulikua mnataka vita Katika taifa la Kenya. Lakini sisi kama Kenya Kwanza tulisimama imara na tukahubiri amani na siasa imeisha. County commissioner ujipange my friend, lazima uende nyumbani."