Sijashuhudia kisa chochote cha kuwahonga wapiga kura-Malala

Malala, aliwapongeza wakazi kwa kudumisha amani katika uchaguzi unaoendelea wa gavana kakamega.

Muhtasari
  • Malala amesema kuwa hajashuhudia kisa chochote cha kuwahonga wapiga kura, akidokeza kuwa uchaguzi huu ni wa amani
Seneta wa Kakamega Cleophas Malala
Seneta wa Kakamega Cleophas Malala
Image: Screengrab:YouTube

Muwaniaji wadhifa wa Ugavana wa Kakamega Cleophas Malala  amejitenga na madai ya kuwahonga wapiga kura katika uchaguzi wa Ugavana unaoendelea.

Malala amesema kuwa hajashuhudia kisa chochote cha kuwahonga wapiga kura, akidokeza kuwa uchaguzi huu ni wa amani.

Alitoa wito kwa viongozi kukoma kuwachochea wakazi kwa kutoa matamshi ambayo hayana msingi, akiwataka walio na malalamishi kuripoti kwa afisi husika.

Malala, aliwapongeza wakazi kwa kudumisha amani katika uchaguzi unaoendelea wa gavana kakamega.

“Tumeshuhudia hali ya amani, nawashukuru watu wa Kakamega kwa kushiriki ucaguzi wa amani. Ni muhimu kwa wakazi kuruhusiwa kupiga kura kuwachagua viongozi wao,” alisema Malala.

Aidha alitoa wito kwa wapiga kura kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo.

Malala alisema atakubali kushindwa iwapo uchaguzi hautakumbwa na changamoto huku akitoa wito kwa wapinzani wake kukubali matokeo.