Uhuru afanya mkutano wa faragha na magavana waliochaguliwa wa ODM

Mkutano huo ulifanyika Jumatatu katika afisi ya gavana wa Mombasa anayeondoka Hassan Ali Joho.

Muhtasari

•Rais Uhuru Kenyatta alifanya mkutano wa faragha na viongozi wapya waliochaguliwa huko Mombasa na Kilifi kwa tiketi ya muungano wa Azimio-One Kenya.

Rais Uhuru Kenyatta akiondoka kwenye duka la Ice Cream kando ya barabara ya Makadara baada ya kula chakula cha mchana katika mkahawa wa Barka mjini Mombasa katika picha hii iliyopigwa tarehe 31 Agosti 2022.

Image: LABAN WALLOGA

Rais Uhuru Kenyatta alifanya mkutano wa faragha na viongozi wapya waliochaguliwa huko Mombasa na Kilifi kwa tiketi ya muungano wa Azimio-One Kenya.

Mkutano huo ulifanyika Jumatatu katika afisi ya gavana wa Mombasa anayeondoka Hassan Ali Joho.

Waliohudhuria mkutano huo ni gavana anayeondoka wa Mombasa Hassan Joho, Gideon Mung'aro (Kwale), gavana mteule wa Mombasa Abdulswamad Nassir pamoja na naibu wake Francis Thoya.

Maelezo ya mkutano huo hayakufichuliwa kwa kuwa vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia.

Baada ya mkutano, viongozi walienda katika mgahawa wa Barka kwa chakula cha mchana.