logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maswali magumu yaliyoulizwa na majaji wa mahakama ya juu

Majaji waliwauliza mawakili wa Ruto na wa IEBC maswali magumu ambayo wanapaswa kuyajibu Jumamosi alfajiri.

image
na SAMUEL MAINA

Uchaguzi02 September 2022 - 04:58

Muhtasari


  • •Mawakili wa mlalamishi Raila Odinga wanatazamiwa kujibu maswali walioulizwa na majaji wa Mahakama ya Juu.

Kesi ya kupinga uchaguzi wa rais mteule William Ruto katika mahakama ya Juu nchini Kenya imeingia siku yake ya 3, huku mawakili wa mlalamishi Raila Odinga wakijibu maswali walioulizwa na majaji wa Mahakama hiyo hapo Jana jioni.

Mbali na kujibu maswali hayo mawakili wa William Ruto Pamoja na wale wa IEBC walijibu malalamishi yaliowasilishwa na mawakili wa Raila Odinga Pamoja na mawakili wa makamishna wanne waliojitenga na matokeo hayo.

Na baada ya fursa hiyo kukamilika mwendo wa jioni majaji wa mahakama hiyo wakiongozwa na jaji mkuu Martha Koome waliwauliza mawakili wa bwana Ruto Pamoja na IEBC maswali magumu ambayo wanapaswa kuyajibu hapo kesho alfajiri

Haya hapa ni baadhi ya maswali yalioulizwa na majaji hao

Jaji Ouko

Jaji Ouko kwa Wakili Mahat Somane: Kulikuwa na madai kwamba tofauti ya kura 33,000 iligunduliwa. Ni Kura ngapi zinazoshirikisha zilizopotea? Je, kuna matukio ambapo wapiga kura waliingia kwenye vituo vya kupigia kura na kuwapigia kura wagombea wa Urais pekee?

Jaji Njoki Ndungu

Njoki Ndungu kwa timu ya wanasheria wa IEBC wakiongozwa na wakili Githu Muigai

Je, nini kingetokea ikiwa mwenyekiti wa IEBC angetangaza matokeo yasiyo sahihi? Je, jukumu la makamishna wengine (IEBC) ni lipi?

Jaji Smokin Wanjala

Jaji Smokin Wanjala kwa wakili Karori: Je, jukumu la makamishna wengine wa IEBC ni lipi? Uangalizi ni nini?

Kwa Wakili Mahat: Je, mfumo wa IEBC uliingiliwa naraia wa Venezuela? Je, Raia wa Venezuela alikuwa akidumisha nini kwenye seva ya IEBC?

Je, idadi ya wapiga kura ina umuhimu gani katika kupata 50% pamoja na kura moja ya mgombea?

Je, tuchukulie kuwa kufikia wakati Bw Joseph Kinyua alipokuwa akitoa mwito wa kutaka matokeo ya uchaguzi yamuunge mkono Bw Odinga, je walijua matokeo?

Jaji Smokin Wanjala kwa timu ya wanasheria wa IEBC: Kwa nini mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hakujumuisha matokeo ya maeneo bunge 27 kwenye kura ya mwisho ikiwa yalikuwa yamethibitishwa?

Jaji Philomena Mwilu

Jaji Philomena kwa timu ya Githu Muigai. Je, majukumu ya kikatiba ya makamishna sita wa IEBC ni yapi?

Maoni kuhusu kuondoka kwa makamishna wanne wa IEBC karibu wakati huo huo mwenyekiti (Wafula Chebukati) alikuwa karibu kutangaza matokeo. Je, kuondoka kwao kunamaanisha chochote chini ya Kifungu cha 140?

Je, kuahirishwa kwa uchaguzi wa magavana na maeneo bunge kuliathiri uchaguzi wa rais? Ikiwa waliathiriwa, kwa njia gani?

Philomena Mwilu kwa timu ya mawakili wa IEBC: Kuna mtu fulani aliwataja makamishna 4 wa IEBC kama watetezi, kwa jina lolote lile, wanasalia kuwa makamishna. Kuna hati ya kiapo kwamba wanaegemea upande mmoja. Je, kamishna anapaswa kuchukua nafasi gani? Je, wakiegemea upande mmoja, mahakama ifanye nini?

Jaji Mkuu Martha Koome

Jaji Mkuu Martha Koome kwa timu ya mawakili wa tume ya IEBC: Je, kuna tofauti kutoka kwa IEBC? Jukumu la IEBC ni kuendesha na kusimamia uchaguzi. Kwa nini mwenyekiti wa IEBC aliwagawia makamishna 'kazi za nyumbani' kinyume na shughuli kuu kulingana na Katiba.

CJ Koome kwa timu ya wanasheria wa IEBC: Kwa nini utiririshaji wa moja kwa moja wa matokeo ya uchaguzi wa urais ulikwama?

CJ Koome kwa wakili Mahat: Onyesha jinsi Fomu 34A katika hati za kiapo za walalamikaji zilivyobadilishwa kwa kupigwa picha.

Katika Kujibu maswali hayo Kiongozi wa mawakili wa IEBC Githu Muigai aliwaomba majaji hao kuwapatia muda mawakili wanaopaswa kujibu maswali kujiandaa ili kuyajibu mapema hapo kesho siku ya Ijumaa.

Hatua hiyo ilimlazimu jaji Mkuu Martha Koome kusitisha kikao hicho hadi kesho Ijumaa.

Majaji wa mahakama ya juu hapo jana Jioni waliwauliza maswali kama hayo mawakili wa mlalamishi Raila Amolo Odinga ambao walipata muda wa kujiandaa na kuyajibu mapema leo siku ya Alhamisi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved