Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imetangaza Disemba 8, 2022 kuwa tarehe ya uchaguzi mdogo wa seneta katika kaunti ya Bungoma.
Mwenyekiti Wafula Chebukati alitangaza kupitia notisi ya gazeti la serikali.
"Uchaguzi Mdogo wa Mwakilishi wa Seneti, Kaunti ya Bungoma Umeratibiwa kufanyika tarehe 8 Desemba 2022," alisema.
Kiti cha useneta wa Bungoma kiliachwa wazi kufuatia kuchaguliwa kwa Moses Wetangula kama spika wa Bunge la Kitaifa.
Alikuwa amehifadhi kiti hicho kwa muhula wa tatu.
Alisema kuwa uchaguzi mdogo katika wadi za Ololmasani, Kyome/Thaana, Utawala, Mumias Kaskazini na Gem Kusini pia utafanyika tarehe hiyohiyo.
Uchaguzi katika wadi hizi uliahirishwa baada ya baadhi ya waliokuwa wakiwania viti hivyo kufariki kabla ya uchaguzi kufanyika.