Lonyangapuo abwagwa chini na Kachapin wa UDA katika kinyang'anyiro cha ugavana West Pokot

Kachapin alikuwa amepoteza kwa Lonyangapuo katika uchaguzi wa 2017.

Muhtasari

•Lonyangapuo ambaye amehudumu kwa muhula mmoja alikuwa anajaribu kutetea kiti chake kwa tiketi ya Kenya Union Party (KUP).

•Kachapin sasa anachukua usukani wa West Pokot kwa mara ya pili baada ya kuhudumu muhula wa 2013-2017.

Gavana wa West Pokot anayeondoka John Lonyangapuo
Image: MAKTABA

Mgombea ugavana wa West Pokot kwa tiketi ya UDA Simon Kachapin ametangazwa mshindi baada ya hesabu za kura katika kaunti hiyo kukamilika.

Tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC) imesema kuwa Kachapin alishinda kiti hicho kwa kura 86,476 na kumbwaga chini gavana anayeondoka John Lonyangapuo ambaye alipata kura 84,610.

Lonyangapuo ambaye amehudumu kwa muhula mmoja alikuwa anajaribu kutetea kiti chake kwa tiketi ya Kenya Union Party (KUP).

Naibu gavana anayeondoka Nicholas Atudonyang pia alikuwa anamezea kiti hicho kwa tiketi ya KANU.

Kachapin sasa anachukua usukani wa West Pokot kwa mara ya pili baada ya kuhudumu muhula wa 2013-2017.

Gavana huyo mteule alipoteza  kwa Lonyangapuo katika uchaguzi wa 2017. Wakati huo Kachapin alikuwa akijaribu kutetea kiti chake kwa tiketi ya Jubilee huku Longangapuo akiwania kwa tiketi ya KANU.