Makamishna wawili na Mkurugenzi Mtendaji wa IEBC wamejeruhiwa- Chebukati

Chebukati alisema ametishwa, lakini ana jukumu la kuwatumbuiza Wakenya.

Muhtasari

•Mweneyikiti wa IEBC Wafula Chebukati alibainisha kuwa baadhi ya wafanyakazi wake pia wameathirika.

akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 10, 2022
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 10, 2022
Image: ENOS TECHE

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati sasa anasema wawili wa kamishna wake na Mkurugenzi Mtendaji wa IEBC wamejeruhiwa na kwa sasa wanapokea matibabu hospitalini.

Akizungumza siku ya Jumatatu kabla ya kutangaza matokeo ya urais, Chebukati alibainisha kuwa baadhi ya wafanyakazi wake pia wameathirika.

Alidai kuwa baadhi walikamatwa kutoka kituo cha kitaifa cha kujumuisha kura kilichopo Bomas na hakuna sababu zilizotolewa kwa ajili hiyo.

"Haikuwa safari rahisi, hivi sasa makamishna wangu wawili na Mkurugenzi Mtendaji wamejeruhiwa na wanatibiwa. Wafanyikazi wetu wametambulishwa. Msimamizi wa uchaguzi eneo la Embakasi Mashariki alitoweka akiwa kazini," Chebukati alisema.

Alisema ametishwa, lakini ana jukumu la kuwatumbuiza Wakenya.

“Tuna watumishi ambao wamekamatwa ovyo bila sababu, wengine wanaunda kituo hiki lakini tuna wajibu wa kikatiba kufanya kazi ndiyo maana nasimama mbele yenu licha ya vitisho.