(+Video) Wajackoyah amfokea shabiki aliyeshika sehemu zake za siri

"Usinishike hivyo!"... sasa huyu ananishika sehemu yangu ya nyeti!" Wajackoyah alisema.

Muhtasari

โ€ขWajackoyah alilazimika kusimamisha hotuba yake kwa muda baada ya mfuasi wake mmoja aliyesisimka kugusa sehemu zake za siri.

โ€ขWanamitandao walifanya mzaha na tukio hilo wakidai kuwa huenda shabiki huyo aliamua kufuata kauli mbiu ya Root Party chake Wajackoyah,  'Tingiza miti'.

Mgombea urais Wajackoyah,wakati wa mahojiano na Radiojambo 10/juni/2022
Image: CHARLENE MALWA

Unyanyasaji wa kingono sasa unaonekana kumuathiri mtu yeyote bila ubaguzi wakiwemo wagombea urais.

Siku ya Ijumaa mgombea urais wa Roots Party Profesa George Wajackoyah alilazimika kusimamisha hotuba yake kwa muda baada ya mfuasi wake mmoja aliyesisimka kugusa sehemu zake za siri.

Wajackoyah ambaye alikuwa amevalia suruali ya michezo, T-shati ya kijani na durag kichwani kama ilivyo kawaida yake alikuwa amesimama juu ya lori huku akiwahutubia wafuasi wake wakati tukio hilo lilitokea.

"... na mimi nimekuja nikasema.." Wajackoyah alisikika akisema katika klipu ya video inayosambaa kabla ya mguso wa ghafla kwenye sehemu zake za siri kumsimamisha.

"Usinishike hivyo!"... sasa huyu ananishika sehemu yangu ya nyeti!" mgombea urais huyo ambaye alionekana kukerwa na kitendo hicho alisikika akilalamika.

Video ya tukio hilo imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii huku wanamitandao wakitoa hisia mseto.

Baadhi ya wanamitandao walifanya mzaha na tukio hilo wakidai kuwa huenda shabiki huyo aliamua kufuata kauli mbiu ya Root Party chake Wajackoyah,  'Tingiza miti'.

Haya baadhi ya maoni ya wanamitandao:-

@AtCheckmate Shabiki wa kike wa Wajackoyah mwenye kiu aliamua kuweka kauli mbiu yake ya TINGIZA MITI kwa vitendo kwa kumtikisa mwenye kauli mbiu โ€œmitiโ€ YAWA!!??

_law_____ ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ali kua ana angalia kaaa herb iko apo

lushy_puffy_254 Anaskizia penye Roots zinatoka ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

mrbradley__  Tingiza tingiza

steveranker  ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Anataka kucastrate the 6th

trapkidobreezy Tabia mbaya inafanyika kila mahali๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Haya yalijiri siku moja tu baada ya mgombea urais huyo na mgombea mwenzake Justina Wamae kuonekana katangamana na wafuasi wao katika klabu moja jijini Nairobi.

Picha zinazoonyesha wakiwa wamezingirwa na vipusa warembo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuwasisimua wanamitandao.