Mungatana Alitoa Kijasho Kunipata, Asimulia Mwanaisha Chidzuga

rsz_chidzuga
rsz_chidzuga
"Mimi na bwanangu mheshimiwa Mungatana hatukupatana barabarani! Alito kijasho kunipata" mwanahabari mashuhuri nchini, Mwanaisha Chidzuga alisimulia wakti alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa bustani la MJ, Maureen Massawe Jappani.

Mwanaisha ambaye ni mkewe mwanasiasa aliyekuwa mbunge wa Garsen, Danson Mungatana alisimulia jinsi wawili hao walivyopatana huku akifichua kuwa safari ya Mungatana ambaye anajulikana kama 'mla mamba' kujishindia roho ya mpenziwe, haikuwa tu mteremko wa halua na asali bali ilihusisha bidii chungu nzima na jasho si haba.

"Kwa hivyo hamkupatana kwa chumba cha habari?" Aliuliza Massawe.

"Alinitafuta." Alijibu bi Chidzuga."Alitafuta nambari yangu ya simu mpaka akapata akaanza kunitafuta kila mahali, Mombasa lakini wapi hakunipata, na aliponipata haikuwa mambo ya 'nakupenda' alifanya bidii kujishindia mimi. Alifanya kila juhudi kuwai uaminifu wangu." Alisimulia mama wa wana watatu.

Huku akisimulia, swala lililojitokeza wazi ni swala la uhusiano na changamoto ambazo zimekumba ndoa yao huku akifafanua kuwa licha ya madai kuwa yeye ni mke wa pili au wa tatu wa mwanasiasa huyo, yeye ndiye malkia na sio malkia pekee bali hakuna mwingine anayemwita mke mwenza.

"Inasemekana kwamba mda mmoja aliyekuwa malkia wa urembo nchini, Cecilia Mwangi ndiye aliyeingia kwenye ndoa hii kama mke wa tatu wake Mungatana." Aliuliza Massawe.

"Hapana. Vile nitasema ni kuwa ndoa sio rahisi natumai wanawake huku nje wananiskiza, ndoa ni kazi na katika ulimwengu hakuna mtu aliyekamilika kumliko mwingine na duniani sasa kuna majaribio mengi na mengi hutokea, lakini swala ni kipi unachofanya kurauka dhidi ya hayo yote?." Alijibu Chidzuga, mwanamke mrembo kupindukia.

"Lakini kitu kimoja ni; mwanamume akija kwako na akiri kuwa alikosea na aombe msamaha na aombe usaidizi wa kurekebisha makosa yake na ana bidii ya kurekebisha aliyokosea, unampa fursa ya pili. Alistahili fursa ya pili." Do! aliongeza mwanahabari huyo ambaye licha ya kuolewa na mwanasiasa, amelelewa katika familia ya kisiasa huku mamake, Zainab Chidzuga akiwa mwanasiasa ambaye ni mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Kwale.

Chidzuga pia aliongelea mengi kuhusu dhana ya kwamba wanawake au kinadada walioko katika vyombo vya habari wanapenda sana kuwa katika uhusiano na wanasiasa, huku pia akifichua mbona kamwe hawezi mhoji bwanake katika runinga.

Skiza kanda ifuatayo.