Mama yangu ananiambia niende Saudi Arabia nikafanye kazi licha ya mimi kuwa kwenye ndoa-Mwanamke asimulia haya

Muhtasari
  • Mama yangu anamdharau mume wangu kwa maana hana mali ananiambia nitafute kazi ili nimletee pesa
  • Nimekuwa nikichukua mikopo ili nimsaidie, hatambui masomo bali anatambua pesa
sad woman
sad woman

Mwanamke mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo baada ya kufichua masaibu ambayo amekuwa akipitia baada ya mama yake kumdharau mumewe kwa maana hana pesa.

Mwanamke huyo alisema kwamba mama yake hakutambua elimu bali alitambua pesa na amekuwa akishauri anapaswa kutoka kwa ndoa yake na kuanza kufanya kazi.

Kulingana na mwanamke huyo amekuwa akichukua mikopo ili kumtumia mama yake aache kuteta kwa ajili ya ndoa yake.

 

"Mimi nimekuwa kwa ndoa kwa zaidi ya miaka kumi, nina watoto watatu, mume wangu alisimamishwa kazi wakati huu wa corona

Nimekuwa nikifanya vibarua ili tuweze kujikiu, kifungua mimba wangu yuko katika chuo kikuu,mama yangu amekuwa akimdharau mume wangu kwa maana hana pesa

Nikimuuliza kwanini anataka niende kufanya kazi ananiambia mume wangu hakumpelekea mahari kwa hivyo hiyo si ndoa, aliniambia nitoke kwa ndoa niende Saudi Arabia nikafanye kazi nimletee pesa

Hakutambua elimu ni nini anataka tu pesa." Alieleza Mwnamke huyo.

Pia alisema kwamba hajui afanya aje kwa maana hawezi kuwaacha wanawe na amekuwa kwa ndoa kwa miaka mingi.

Je ni vyema waazi kuingilia maisha ya ndoa ya watoto wao?

Je ushauri wako kwake ni upi?