Mke wangu amekuwa akitoka kwa ndoa anakaa na mwanamume mwingine kisha anarudi-Mwanamume alia

Muhtasari
  • Mwanamume aeleza masaibu ambayo amepitia mikononi mwa mkewe

Mwanamume mmoja aliyefahamika kama Wanjohi aliwaacha mashabiki wa radiojambo mdomo wazi baada ya kutaka ushauri kutokana na tabaia za mkewe.

Kulingana na Wanjohi alisema kwamba mkewe amekuwa akiacha ndoa yake anaenda kuolewa na mwanamume mwingine na kumuachia mumewe watoto.

Baada ya muda mkewe anarudi na kisha anaendelea na maisha na mumewe.

 

"Mke wangu amekuwa ananiachia watoto wetu anaenda anaolewa tena baada ya muda anarudi tunaishi pamoja, akifika kwa mwanamume huyo anampa simu tunazungumza naye

Kuna wakati aliniachia mtoto wa mwaka mmoja, nilipooa alirudi na mwanamke huyo akaenda,akirudi kwa maana mimi ni mwanamume muungwana hatuendi kupimwa virusi vya ukimwi tunaendelea hivyo

Wiki iliyopita mke ambaye nilioa alienda kumembelea mama yangu alipofika sokoni aliyekuwa mke wangu alikuwa eneo hilo, alipowaona na watotowalipga nduru na kusema kuwa mke wangu ameiba watoto wake

Mwanamume ambaye alimuoa alimchapa mke wangu watoto wangu walimkataa na kusema kuwa wanataka huyo ke wangu wa pili." Alieleza.

Je Unaweza kumpa bwana huyo ushauri upi kulingana na masaibu ambayo yanamkumba?