Nilipogundua mume wangu ananidanganya,nilimdanganya na wanaume 3-Muigizaji Njambi

Muhtasari
  • Studioni katia kipindi cha ilikuaje tulikuwa na muigizaji Njambi ambaye alizungumzia vurugu vya nyumbani ambavyo alipitia katika ndoa yake ya awali
Njambi
Image: studio

Studioni katia kipindi cha ilikuaje tulikuwa na muigizaji Njambi ambaye alizungumzia vurugu vya nyumbani ambavyo alipitia katika ndoa yake ya awali.

Njambi alisema kwamba aligundua mumewe anadanganya, hii ni baada ya kuenda kwa wiki mzima akirudi anamwambia kwamba ametoka baa, ilhali hakuwa anapokea simu zake.

"Mume wangu alikuwa anatoka kwa nyumba kwa wiki mzima, nikimpigia simu hapokei, akirudi nyumbani ananiambia kwamba ametoka baa

 

Niligundua kwamba anatoka nje ya ndoa, na mimi nikaamua kumdanganya na wanaume watatu, pia alijua kwamba natoka nje ya ndoa, siku moja alirudi nyumbani na kuniuliza kama hamna kiberiti nilimwambia kwamba iko jikoni

hapo nilitoroka, nilienda kujificha chini ya gari, alinichapa lakini niliokolewa na majirani,niliporudi kwetu baba yangu aliniambia asiwahi sikia kwamba nimerudi kwa huyo mwanamume," Alizungumza NJambi.

Njambi aliwahimiza wakenya wapendane licha ya changamoto ambazo wanapitia.

Muigizaji huyo pia alifichua kwamba alipokuwa chuo kikuu aliwachumbia 'sponsor' si kwa ajili wazazi wake hawanempa pesa bali kwa ajili ya shinikizo kutoka kwa marafiki.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube.