Maajabu!Mbuzi na kuku wamtembelea mmiliki wao hospitalini baada ya kulazwa Kitui

Muhtasari
  • Mbuzi na kuku wamtembelea mgonjwa hospitalini Kitui
  • Kulingana na Ghost Kuku na Mbuz hao walienda kumtembelea,mmiliki wao baada ya kulazwa hospitali akiwa mgonjwa
Mtangazaji Ghost Mulee
Image: Hisani

Katika kitengo cha story za Ghost alisimulia jinsi mbuzi na kuku waliwashangaza madaktari katika hospitali moja kaunti ya Kitui.

Kulingana na Ghost Kuku na Mbuzi hao walienda kumtembelea,mmiliki wao baada ya kulazwa hospitali akiwa mgonjwa.

Kaunti hiyo ilivuma mapema mwaka huu baada ya mamba mmoja kumwangukia na kumuuma dereva wa lori kutoka juu.

"Katika kaunti ya Kitui, mbuzi na kuku waliwashangaza madaktari na watu baada kuingia hospitali

Mbusi aliingia kwenye eneo la mapokezi, kisha kuku wakafuata, walienda mpaka wadi ambayo mgonjwa wao alikuwa amelazwa

KUku hao walipanda mpaka kitandani alipo kuwa mgonjwa huyo, ilhali mbuzi allikuwa kando ya kitanda hicho."