logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Stori za Ghost: Mhubiri afurushwa kanisani na waumini baada ya kupiga marufuku sadaka ya Sh50

Mhubiri huyo alilalamika kuwa hamsini ni pesa kidogo sana ambazo haziwezi kusaidia katika maendeleo ya kanisa.

image
na Radio Jambo

Habari18 October 2021 - 05:55

Muhtasari


•Mhubiri huyo alilalamikia kitendo cha baadhi ya waumini kukosa kutoa sadaka na wengine kutoa sadaka ya chini ya shilingi 50.

•waumini wa kanisa hilo hawakupendezwa na hatua ya mhubiri wao na wakaanza kumzomea hadi akakimbia kuenda kusikojulikana.

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha 'Stori za Ghost' mtangazaji Ghost Mulee alisimulia kisa ambacho kilitokea katika kanisa moja eneo la Mshomoroni kaunti ya Mombasa.

Kulingana na Ghost, Mhubiri mmoja alijpata mashakani baada ya waumini kughadhabishwa na hatua yake ya kupiga marufuku sadaka ya shilingi hamsini.

Mhubiri huyo alilalamikia kitendo cha baadhi ya waumini kukosa kutoa sadaka na wengine kutoa sadaka ya chini ya shilingi 50.

"Nimekuwa na nyiynyi kwa muda mrefu sana lakini kanisa letu haliendelei. Sababu ni kuwa ukiangalia wengine wetu wanatoa sadaka, wengine hawatoi. Kuanzia leo mimi nimepiga marufuku sadaka ya shilingi 50" Mhubiri aliambia waumini.

Mhubiri huyo alilalamika kuwa hamsini ni pesa kidogo sana ambazo haziwezi kusaidia katika maendeleo ya kanisa.

Hata hivyo waumini wa kanisa hilo hawakupendezwa na hatua ya mhubiri wao na wakaanza kumzomea hadi akakimbia kuenda kusikojulikana.

"Waumini walijiuliza, 'pasta kavuta bangi nini?' Mhubiri akajaribu kuwaeleza kuhusu miradi wakamwambia kwamba hata nguo alizovaa zilinunuliwa kwa sadaka ambayo walitoa. Walimwambia kuwa hana mamlaka ya kumlazimisha mtu kutoa kiwango fulani cha sadaka.Mhubiri hata hakumaliza ibada, alitoka akaenda zake" Ghost aisimulia.

Ghost aliwasihi wahubiri wote kukubali sadaka ya waumini jinsi tu ilivyo bila kulalamika, iwe ndogo iwe kubwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved