Mwanadada kwa jina la Faith anasema jamaa mmoja waliyekuwa katika mahusiano ya kimapenzi alimkwepa kabla ya kupata mimba na hajawahi shughulikia mtoto wake ambaye sasa ana miaka mitatu.
Walikuwa wamekaa pamoja kwa mwezi ila baada ya jamaa kubaini ameshika ujauzito, alimtafutia njia ya kumkwepa kwa kumtuma nyumbani kwao.
Mwanadada huyo anaeleza jahazi lilianza kuzidiwa na mawimbi baada ya familia yake kumtia kijana wa watu jela kwa kumpa ujauzito akiwa bado shule.
“Nilikuwa bado niko shule na baada ya mamangu kugundua akakasirika na kutuweka ndani. Ilibidi familia yake wameuza mpaka shamba ili wamtoe ndani na sasa mama yake akawa na hasira na kusema kwamba akiniona ataniuwa,” Faith alielezea Massawe.
Wawili hao walifungwa jela kwa muda baada ya wazazi wa msichana kubaini kwamba amepata mimba ya kijana huyo, hali iliyopelekea familia ya mvulana kuuza shamba ili kumtoa mwanao ndani na huo ukawa ndio mwanzo wa msukosuko wa mahusiano yao.
Msichana anaeleza kwamba baada ya kutoka jela, alimwambia msichana kwamba anaelekea jijini Nairobi kutafuta ajira ili baadae amuite waishi pamoja ila hili halikutimia kwani siku moja msichana alijaribu kumpigia simu mvulana huyo kwa hasira akamtukana pamoja na wazazi wake.
Mvulana huyo kwa jina Stirius baadae alioa na akamtelekeza mpenzi wake wa awali pamoja na mtoto wake.
Mvulana huyo anadai kutomshughulikia mtoto wake kunatokana na wazazi wake kutokuwa na maelewano na wazazi wa msichana.