logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sio mara ya kwanza madaktari kusema sina muda wa kuishi-Akuku Danger afunguka

Pia alisema kwamba mama yake aliaga dunia mwaka wa 2012

image
na Radio Jambo

Vipindi26 April 2022 - 11:30

Muhtasari


  • Pia alisema kwamba mama yake aliaga dunia mwaka wa 2012 alipokuwa anajiunga na chuo kikuu

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye mchekeshaji Akuku Danger ambaye aliugua kwa muda wa zaidi ya miezi 3.

Huku akizungumzia ugonjwa aliokuwa anaugua 'sickle cell Anemia' Akuku Danger alisema kuwa;

"Baada ya kuamka baada ya kuwa kwenye Coma kwa siku nne, sikuwa natambua watu hata sikuweza kutambua baba yangu na dada yangu, kwani akili yangu ilikuwa bado niko nyumbani

Madaktari waliambia familia yangu kwamba sitaisi ata niekewa kwenye mashine ni pesa na wakati wao wanaharibu na kuwa wanapaswa kunipa tu masaa

Dada yangu na baba yangu walisisitiza niwekwe kwenye mashine, sio mara ya kwanza mdaktari kusema kwamba nina masaa tu ya kuishi, nikiwa darasa la tano niligonjeka na madaktari wakamwambia mama yangu kwamba anapaswa kunipa masaa nikufe kwa hivyo anirudishe nyumbani," Alizungumza Akuku Danger.

Pia alisema kwamba mama yake aliaga dunia mwaka wa 2012 alipokuwa anajiunga na chuo kikuu.

"Wakenya walinisaidia sana, upendo wao na watu ambao hawanijui wakanichangia, niko kwenye uhusiano na Sandra Dacha, tumekuwa kwenye uhusiano kwa miezi saba, nina mpango wa kumvisha pete ya uchumba," Akuku Alifichua.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved