logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanaume aomba msamaha kwa kumtusi mama na baba mkwe

Titus alitaka kuskizana nao ili wamruhusu kumwona na kuongea na mwanawe

image
na Davis Ojiambo

Vipindi09 December 2022 - 09:15

Muhtasari


  • • Titus alisema kuwa uhusiano wake na mama mkwe ulikuwa ukiyumbayumba kuanzia hapo awali ila yeye ndiye aliyezidisha ugomvi naye.
  • • Mama mkwe alisema kuwa Titus amekuwa akiwasumbua akitaka kuona mtoto wake kwa madai kuwa baba yake amekufa na angetaka bintiye ahudhurie matanga ili afahamike nyumbani.

Katika kipindi cha Gidi na Ghost, kitengo cha Patanisho, Bwana Titus alituma ujumbe akitaka kupatanishwa na mama mkwe wake, Sofia Akeya.

Titus alisema kuwa uhusiano wake na mama mkwe ulikuwa ukiyumbayumba kuanzia hapo awali ila yeye ndiye aliyezidisha ugomvi naye.

"Nilipatana na msichana Nairobi, tukapata mtoto wa kwanza kisha akafa. Mama mkwe akaja akamchukuwa . Alipoenda naye, alikaa miezi miwili akarudi," Titus alisema.

Alisema kuwa baada ya muda mamake msichana alipiga simu na kusema kuwa anataka kumrudisha shuleni na akarejea nyumbani.

Hata hivyo, msichana aliporudi, hakurudishwa shule, alipelekwa kufanya kazi ya nyumba ila badaye hawakuskizana na mwenye nyumba ikabidi Titus amwendee.

"Baada ya kumwendea tulipata mtoto wa pili, mama yake akamtishia ikabidi arudi nyumbani akiwa na ujauzito.Nilikuwa namtumia pesa 2500 kisha mama mkwe akasema pesa hiyo ni kidogo. Hataki niongee na mtoto," baba huyo alisema.

Titus alisema kuwa nia yake ni kumshughulikia mwanawe na hata kujua iwapo ameenda shuleni.

Mama Sofia alisema kuwa Titus na bintiye walipatana akiwa tu amemaliza kidato cha 4 na baada ya mwanao kufa hawakuwa na njia ya kumzika.

Alisema kuwa mume wake alimfahamisha hayo kisha wakapanga ndipo mtoto akazikwa ila baada ya hapo mambo yaliharibika.

"Alinitukana akaniambia mimi ni malaya, mjinga, msichana akatoka huko akiwa mjamzito, hajui mtoto anakula nini anavaa nini anakunywa nini, anatusi kila mtu akiwemo mume wangu. Hajawai tuma pesa, hata kitabu wala kalamu, mwambie ajiheshimu ili mimi nimheshimu," Sofia alisema.

Aliongeza kuwa Titus amekuwa akiwasumbua akitaka kuona mtoto wake kwa madai kuwa baba yake amekufa na angetaka bintiye ahudhurie matanga ili afahamike nyumbani.

Hata hivyo, alikuwa amekereka na tabia ya Titus ambayo si ya heshima na kusema kuwa hda baada ya kitengi cha Patanisho bado atamtusi.

"Mambo yake sitaki kuyasikia, mtoto si mzigo,nimelea watoti sita, hukufundishwa na wazazi wako adabu, unaniweka hewani ukijua huna tabia,unatusi mume wangu, msichana wangu na hata mwanangu," mama mkwe alisema.

Alimaliza akisema kuwa hataki kujihusisha na Titus na atamlea mtoto bila usaidizi wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved