Stori za Ghost:Mzee wa miaka 69 afika mahakamani kuomba umri upunguzwe kuwa 49

Mahakama imemwambia mzee huyo kwamba itampa jibu baadaye.

Muhtasari

•Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 69 alifika mbele ya mahakama akiomba kuruhusiwa kubadilisha umri.

•Mzee huyo sasa anaomba mahakama imruhusu awe na miaka 49 kwani anatamani sana kurejea kazini.

Ghost Mulee studioni
Ghost Mulee studioni
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, mtangazaji Jacob 'Ghost' Mulee alisimulia tukio moja ambalo lilitokea Uholanzi.

Kulingana na Ghost, mzee mmoja mwenye umri wa miaka 69 alifika mbele ya mahakama akiomba kuruhusiwa kubadilisha umri.

Mzee huyo alitaka mahakama kuondoa miaka ishirini kutoka kwa umri wake halisi na kuamua kuwa ana miaka 49.

"Kuna jamaa mmoja wa miaka 69 ameenda mahakamani. Ameambia jaji kwamba anataka kuwa 69," Ghost alisimulia.

Ghost alieleza kuwa mwanamume huyo aliteta kuwa ikiwa watu wanaruhusiwa kubadilisha mambo mengine ya kibinafsi kama vile majina na jinsia, basi mtu pia anafaa kuruhusiwa kubadilisha umri.

"Anateta kuwa katika umri wake wa sasa amezuiliwa. Anasema ameshindwa kupata kazi nzuri katika umri wake, hawezi kupata mchumba wa miaka sawa na anayotaka na nafasi zake za kuajiriwa zimepungua," 

Mzee huyo sasa anaomba mahakama imruhusu awe na miaka 49 kwani anatamani sana kurejea kazini.

Kulingana na Ghost, mahakama imemwambia mzee huyo kwamba itampa jibu baadaye kwa kuwa jaji bado hajapata jibu halisi.