Mtangazaji Gidi atoa taarifa kuhusu afya yake baada ya kushambuliwa na ugonjwa

Mashabiki wa Gidi na Ghost asubuhi walikosa sauti ya Gidi siku ya Alhamisi na Ijumaa.

Muhtasari

•Gidi anaendelea kupata nafuu baada na kushambuliwa na maradhi yasiyothibitishwa kwa siku chache zilizopita.

•Alhamisi, Ghost alifichua kuwa mwenzake amechukua mapumziko mafupi na akadokeza angerejea Jumatatu.

anaendelea kupata afueni baada ya kuugua
Mtangazaji Gidi Ogidi anaendelea kupata afueni baada ya kuugua

Mtangazaji wa Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo, Gidi Ogidi ametoa taarifa kuhusu afya yake.

Gidi anaendelea kupata nafuu baada na kushambuliwa na maradhi yasiyothibitishwa kwa siku chache zilizopita.

Jumamosi asubuhi, mtangazaji huyo mahiri alichapisha picha yake akiwa katika chumba cha wagonjwa cha hospitali huku akiwa na sindano kwenye mkono wa kushoto na kuthibitisha kwamba anahisi vizuri zaidi.

"Siku ya tatu ya sindano ya IV, nahisi vizuri zaidi," alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Mwanamuziki huyo wa zamani aliendelea kuwatakia mashabiki wake Sabato njema.

IV ni mbinu ya kimatibabu inayotumiwa kutia maji, dawa na virutubisho moja kwa moja kwenye mshipa wa mgonjwa. Inatumiwa kwa wagonjwa wengi waliolazwa katika hospitali na magonjwa mbalimbali.

Mashabiki wa kipindi maarufu cha Gidi na Ghost Asubuhi Radio Jambo asubuhi walikosa sauti ya Gidi siku ya Alhamisi na Ijumaa huku mtangazaji mwenzake Ghost Mulee akiendesha kipindi hicho peke yake.

Siku ya Alhamisi, Ghost alifichua kuwa mwenzake alikuwa amechukua mapumziko mafupi na akadokeza kuwaa angerejea siku ya Jumatatu wiki ijayo.

"Leo hatupo na bosi wangu. Kesho (Ijumaa) pia hatutakuwa naye. Bosi wangu amechukua mapumziko kidogo. Natumai tutakuwa naye Jumatatu," Ghost alisema wakati wa kipindi cha asubuhi cha Alhamisi.

Mashabiki wa Gidi wameendelea kumtakia afueni ya haraka chini ya taarifa yake ya Instagram aliyotoa Jumamosi.

nyambaremph: Quick recovery bro

kitmikayi78: Happy Sabbath to you too. It will be well God is in control.

layieta: Speed recovery Gidi. Our Radio Jambo mafia.

Faithkamui: Pole Gidi, get well soon

thomas.mukoya Quick recovery bro. Keep the faith

Sote katika Radio Jambo tunamtakia mtangazaji huyo wetu tumpendaye neema ya Mola na afueni ya haraka.