Katika kitengo cha Patanisho, Asman Abande (34) alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Amina Namale (32) ambaye alikosana naye mwaka jana.
Asman alisema mkewe aligura ndoa yao ta miaka 8 Desemba mwaka jana baada ya kumpiga kwa kuhudhuria matanga bila idhini yake.
Alidai kwamba alimkataza mkewe kuhudhuria matanga ya mama ya aliyekuwa mpenzi wake ila akasisitiza kuenda.
"Mke wangu alikuwa na ex wake. Mama ya ex wake akafa, akaniambia anataka kuenda matanga nikamkataza. Akasema lazima aende, akaenda. Aliporudi nikampiga. Alikasirika akaenda kwao," Asman alisimulia.
Alieleza, "Nilimkataza kwa sababu bado alikuwa na mahusiano na huyo kijana. Tuko na watoto wawili na yeye. Kitambo ni kama alikuwa amepata mimba yake lakini akatoa. Nilipata amepeleka watoto kwa wazazi wake."
Aidha, alifichua kuwa baada ya kumpiga mkewe, aliwatuma ndugu zake kumpiga ila kwa bahati nzuri akasaidiwa na majirani.
"Siku nilimpiga alituma vijana wao kuleta vita. Watu waliposikia kelele wakakuja kusaidia," Azman alisema.
Asman alisema kwamba angependa kujua msimamo wa mzazi huyo mwenzake ili aweze kujua hatua ya kuchukua.
Bi Amina alipopigiwa simu alimwagiza mumewe apige hatua ya kuenda nyumbani ili waweze kusuluhisha mzozo wao.
"Kama alishindwa kuenda nyumbani kusuluhisha maneno hiyo ni yake. Mtu akisema hawezi kukanyanga kwetu tunaongea nini na yeye? Babangu alimwambia aende nyumbani watengeneze maneno lakini yeye akaenda Nairobi," Amina alisema
Aliongeza, "Alikuwa amezoea kunipiga. Mandugu zangu walienda kwake kumtishia, sio kumpiga."
Asman alijitetea kwa kusema anahofia kuwa akichukua hatua ya kwenda kwa wakwe zake huenda ndugu za mkwe wakampiga.
"Naogopa kuenda huko kwa sababu naweze kuenda nipigiwe huko. Pia nikiwaambia watu wanipeleke wanakataa wakisema hawataki kupigiwa huko," alisema.
Asman alimuomba radhi mkewe na kueleza kwamba anaumia kuwa mbali naye.
Amina alifichua kwamba mzazi huyo mwenzake alidai ameoa mwanamke mwingine baada ya yeye kuondoka.
"Nilimwambia niko na hasira nikitulia nitarudi. Baada ya kukaa siku kadhaa alinipigia akaniambia ameshidwa kuvumilia na amepata mwanamke wa kuoa. Alisema hawezi kurudia matapishi. Alipost mwanamke kwenye Facebook na akaambia dada zake kuwa anataka akuoa. Aliweka picha ya mwanamke huyo na kuandika 'tafakari ya babu'," Amina alisimulia.
Amina pia alitupilia mbali tetesi za kuwa na mahusiano na ex wake huku akieleza kuwa wao ni marafiki tu
"Akiona nalike huyo ex kwenye Facebook nasikia vibaya. Huyo ex ni wa area moja na kwetu. Nilienda matanga juu ya mapenzi ya mama yangu na yeye," alisema.
Alisema, "Ajipange aende nyumbani tuongee. Kama hata hajasaidia watoto hakuna kitu tutaelewana naye."
Asman alimwambia mkewe, "Nakupenda tu sana na sitaki kukaa mbali na wewe ndio maana nimeenda Patanisho."
Amina alisisitiza kuwa anafaa kuenda nyumbani kwao na kuwajibikia watoto ili aweze kufanya uamuzi wa ikiwa atarudi.