logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa amtoroka mkewe kwa madai ya “kelele” nyumbani

Aliwaita Wazee na kuwaambia amechoka na kelele zangu

image
na TOM KIRIMI

Vipindi09 June 2023 - 06:50

Muhtasari


  • •Aliniambia kwamba amesikia maneno huko kwamba nilikuwa nimeoleka kwingine.
  • •Kisha akaita wazee akawaambia amechoka na mimi wazee wakamwambia ni yeye anapaswa kutoka. Ameniblock.
Gidi na Ghost

Katika kitengo cha patanisho, Mary Muthui, 20, ameeleza jinsi alivyotelekezwa na mumewe John Kyalo kwa madai alikuwa ameoleka katika ndoa nyingine kabla ya kuolewa naye.

Katika ujumbe wake redioni Mary ameeleza kuwa, wamekuwa katika ndoa kwa muda wa miaka miwili, alipata ujauzito ambao kwa bahati mbaya ulitoka ila alikiri kwamba tayari anaoujauzito mwingine licha ya kufurushwa na mumewe Mei 26 akiomba kupatanishwa warudiane tena.“Nataka kupatanashwa na Mume wangu anaitwa John Kyalo 21yrs. Tumekuwa kwa ndoa kwa miaka miwili na nilikwa nimepata ujauzito kisha mimba ikatoka. Kwa hivi sasa niko mjazito tena na mimba ya mwezi moja. Tulikosana tarehe 26,5,2023 baada ya yeye kukuja kwa nyumba alafu akaanza kusema kuwa nilikuwa nimetoka kwa ndoa nyingine.” Alisimulia.

“Alikuja kwa nyumba Mei 25, kisha akatoka. Aliniambia kwamba amesikia maneno huko kwamba nilikuwa nimeoleka kwingine, na sikuwa nimeoleka maana alinikujia nyumbani. Hii ni manaeno anapatiwa tuu na watu wenye umbea, kisha akaita Wazee akasema anataka tuachane. Ameniblock.Anasema kuwa anarudi nyumbani akitaka. Mimi nampenda na ningependa arudi nyumbani.” Mary aliendeleza.

Juhudi za Radio Jambo kumpata John kwa njia simu ziligonga mwamba, huku akimwachia Mary mikononi mwa mashauri ya mashabiki kulihusu tukio hilo. Ushauri wako ni upi kwa wapenzi hawa wawili?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved