PATANISHO ; Katika kitengo cha patanisho, Maureen Kambua, 22, ameomba kupatanishwa na bwanake Stephen Mwangi, 23, baada ya kukosana tangu 2020 wakati wa Korona Mwangi alipofika nyumbani akiwa amechelewa.
kulingana na ujumbe wake Maureen, anakiri kukasirishwa na tukio hilo lililochangia kumtusi na hatimaye kutoka kwenda zake. Anajutia tendo hilo, hivyo kuomba kupatanishwa ndipo kuurejesha uhusiano wao.
“Tangu tukosane, nilipoenda kwetu amekaa sana nikimpigia simu hapokei, amenibloki, hadi mwezi Septemba mwaka jana, nilitaka anikujue, amekuwa akinitumia pesa ya mtoto, halafu saa hii nikipigia simu bado hajatukujia, tunachat naye lakini nikimwuuliza atakuja lini kutuchukua, anasema atakuja akipata pesa, nikiongea naye anasema tu ako poa, na hajaoa bibi mwingine tangu nilipotoka,,, anasema hana pesa anajiprepare kutukujia,, hata mtoto nilimpigia picha nikamtumia, lakini haamini huyu mtoto ni wake, mtoto wangu anafanana na motherin law, Mwangi akona wasiwasi na mtoto huyo.” Alieleza Maureen.
Kulingana na mpenzi wake Mwangi, ameeleza kuwa bado angali anapanga kwenda kuwachukua ni vile bado hajapata kazi. Amekiri pia, mkewe alimueleza amepata mimba ila anashuku mtoto huyo si wake akisema iwapo watarudiana lazima wafanyiwe DNA.
“ Nilimwambia angoje kidogo saa hii nimekaa bila job, nilimwambia angoje hadi nipate kazi, ni vyenye nimekaa sana bila kupata kazi, siwezi waendea bila kupata kazi watakuja kutesekea huku bure, nilimwambia avumilie sina shida naye ni vile sa hii sina kazi nilikuambia usiwe na wasiwasi, elewa tu vyenye nakuambia,kama utatukujia haina shida,,Aliniambia amepata mtoto, lakini alikuwa ametoka akaenda kwao, akirudi lazima ataenda DNA .”
Maureen amesema kuwa angetaka kurudi ndipo aishi pamoja na mumewe walee mtoto pamoja,“Nilikuwa nataka kujua msimamo wake, kama atatukujia maana huwa ananiambia atakuja na hakujii, nataka kujua msimamo wako kama utatukujia au unapanga aje”
Ungewashauri vipi wapenzi hawa?