logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kipusa amwaya mtama jinsi alivyomcheza ex wake na nduguye

Mahusiano ya nyakati hizi wengi kama navyosema wanawake wanataka tu pesa kama huna haya basi jua huna mpenzi kamwe.

image
na Radio Jambo

Vipindi05 July 2023 - 16:36

Muhtasari


  • Kipusa mmoja aliwaacha shabiki wa Radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri jinsi alivyomcheza ex wake na ndugu yake.

Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama katika kipindi cha toboa siri ambacho wengi wamemwaya siri zao ambazo wameshindwa kuziweka na wamechomwa nazo.

Kipusa mmoja aliwaacha shabiki wa Radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri jinsi alivyomcheza ex wake na ndugu yake.

Kulingana na kipusa huyo:

"Nataka kumtobolea ex wangu siri ambayo nimeishi nayo kwa muda,tuliachana naye mwezi jana lakini ni mimi nilimuacha,kuna wakati nilienda kumtembelea kwake na kumpata hayuko, hapo ndipo ndugu yake aliweza kucheza kama yeye, tulifanya tendo la ndoa naye,"Alimwaya mtama mwanamke huyo.

Mahusiano ya nyakati hizi wengi kama navyosema wanawake wanataka tu pesa kama huna haya basi jua huna mpenzi kamwe.

Pia kuna wale wanadai kwamba wanaume wengi hawataki kujukumika,kwani pia nao wanataka kuwekwa na wamama ambao wamewazidi umri.

Lakini ukweli ni upi, na uhusiano unahitaji nini ili uweze4 kunawirin kila kuchao na wapenzi kuaminiana.

Asilimia kubwa wanasema kwamba uhusiano unahitajib kujitolea na mwenzi kumwamini mwenzi mwenzake ili uhusiano hudumu.

Lakini wengi wanaona ni kinaya kumwamini mwenzake,kwani warembo zaidi wamo humu nje wakisaka wanaume na wanaume wengi kushinda mwenzi wako wamo humu nje wakisaka wapenzi.

Cha mno ni kwamba ukiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mwamini mwenzi wako na mjue jinsi ya kutatua shida ikitokea.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved