TikToker maarufu Brian Chira ameweka wazi kuwa watu wa jinsia wote walipena kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi naye.
Akizungumza wakati wa mahojiano ya kipekee na Radio Jambo, Chira alibainisha kuwa alikuwa akipokea maombi ya wanaume na wanawake kuwa kwenye mahusiano naye.
"Watu wengi wa jinsia zote, wanaume na wanawake wananitaka kwa sana."
Chira alifunguka hadharani na kukiri kuwa alikuwa anaugua ugonjwa wa Ukimwi na kukanusha uvumi uliokuwa ukienea kuwa amewaambukiza watu virusi hivyo visivyokuwa na tiba na sababu ya hii ilikuwa heshima yake kwa watu wengine.
"Sikuwahi kuambukiza mtu yeyote kama ilivyosemekana na Wakenya mitandaoni maanake nawaheshimu kila mtu katika jamii."
TikToker huyo alifichua kuwa yupo single baada ya mpenzi wake kusitisha mahusiano yao baada ya kupata umaarufu mitandaoni na sababu ya tetesi kuwa akishiriki katika mapenzi ya jinsia moja.
"Niko single sasa hivi, tuliachana na mpenzi wangu baada yangu kuanza kuwa maarufu kwenye mitandao na pia kuskia fununu mimi ni shoga."
Katika mohojino hayo hayo, Chira alieleza jinsi alipata ugonjwa wa Ukimwi.
"kwa njia yenye nahisi rafiki yangu alitumia fursa katika tafrija mjini Mombasa. Kwa namna nyingine naweza nikasema nilibakwa. Na niliripoti kisa hicho niko na ushahidi wa kila kitu, nilirudi hadi chuoni Kabarak nikaripoti nikapewa PrEP… sikupewa maelezo kamili jinsi ya kutumia dawa hizo, nilikuwa natumia mara moja moja kwa kurukisha siku…” alisema.
Kulingana na Chira rafiki yake aliyembaka alijitoa uhai wiki mbili baada ya kumfanyia ukatili huo.