Kwa mara nyingine tena kituo chako pendwa cha Radio Jambo kimerejea na awamu nyingine ya kuwatambua na kuwazawadi wasikilizaji wake kindakindaki kupitia mpango wa ‘Phrase that Pays’.
Mpango huu umekuwa na ufanisi mkubwa katika awamu zilizopita ambapo makumi ya Wakenya wanaosikiliza Radio Jambo walipata kujishindia zawadi za hela kati ya shilingi elfu moja hadi shilingi elfu tano.
Mpango wa ‘Phrase that Pays’ unafanikishwa na mmoja wetu kutembea mitaani kote nchini akiwauliza Wakenya kituo chao pendwa ambacho wanapenda kukisikiliza na kufuatilia vipindi vyake.
Anayeulizwa swali hii akijibu sahihi kwa kusema “Radio Jambo Kituo cha Wakenya” moja kwa moja anajishindia shilingi elfu moja taslimu.
Na ukipatikana umeandika “Radio Jambo Kituo cha Wakenya” kwenye kibango mahali, iwe kwenye kazi yako, kwenye ukuta au bango unatembea nalo barabarani, basi unajishindia takrima ya shilingi elfu tano taslimu.
Kumbuka kauli ya kujishindia hela ni “Radio Jambo Kituo cha Wakenya”!
Sikiliza kituo chako pendwa cha Radio Jambo kila siku ili kujua sehemu aliko mwenzetu wa kukupa takrima akikupata na bango la "Radio Jambo Kituo cha Wakenya".
Hizi hapa ni baadhi ya picha za Wakenya waliopatikana wameandika kwenye mabango “Radio Jambo Kituo cha Wakenya” na kujishindia takrima;